Mwakilishi wa China azitaka nchi zilizoendelea kubeba majukumu zaidi kuchangia fedha UN

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2021

Zhang Jun ambaye ni mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa (UN) mapema wiki hii alitoa wito kwa nchi zilizoendelea kuchukua majukumu zaidi ya kuchangia fedha kwenye chombo hicho cha dunia.

Zhang aliyasema hayo wakati akitoa hotuba kwenye Kamati ya 5 ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa, kamati ambayo ina jukumu kuu la masuala ya fedha na bajeti ya UN.

“Hali ya sasa ya kifedha ya UN inaendelea kubaki yenye mashaka,” Mwakilishi wa China alisema,“Mchangiaji mkubwa wa fedha bado ana malimbikizo ya fedha ambazo hajatoa kwa muda mrefu, kitu ambacho ni chanzo kikubwa cha UN kuwa kwenye hali ya ukata.”

“China inatoa wito kwa nchi wanachama, hususan wachangiaji wakubwa wa fedha, kutekeleza wajibu wao wa kifedha kwa wakati, kwa utimilifu na bila masharti” alisema.

China ikiwa mchangiaji mkubwa nambari mbili katika bajeti ya kawaida na gharama za utunzaji amani duniani, imekuwa ikiwajibika kwa kiwango kikubwa, kulipa gharama za bajeti na ulinzi wa amani na hivi karibuni imelipa ghamara za kulinda amani kama ilivyoelekezwa hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha wa Baraza la Usalama la UN.

“China inatoa wito kwa nchi zilizoendelea kubeba majukumu zaidi ya kuchangia fedha kwa ajili ya UN, na kuchukua kwa uzito changamoto na ugumu unaozikumba nchi zinazoendelea” aliongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha