Sudan yapokea shehena ya kwanza ya chanjo za UVIKO-19 aina ya Pfizer

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2021

Wizara ya Afya ya Sudan wiki hii imepokea shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 zipatazo 499,000 aina ya Pfizer kupitia mfumo wa kidunia wa COVAX ambao ni wa kuwezesha nchi zinazoendelea kupata huduma ya chanjo dhidi ya virusi vya korona.

Dozi hizo za chanjo zimetolewa na Serikali ya Marekani.

Waziri wa Afya wa Serikali ya Sudan Yosra Mohamed Osman alisema katika taarifa yake kwamba “hadi sasa tumeshadunga chanjo kwa zaidi ya raia milioni 1.7.”

Sudan inatarajia kupokea jumla ya dozi za chanjo dhidi ya UVIKO-19 aina Pfizer zipatazo 1,274,130 kufuatia kujenga vizimba vitano vyenye mfumo baridi kwenye eneo maalum la serikali la kuhifadhi dozi za chanjo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha