Abdulrazak Gurnah ashinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2021

(Picha inatoka CRI.)

Taasisi ya Fasihi ya Sweden (Swedish Academy) ilitangaza kuwa, mwanafasihi na mtunzi wa riwaya Abdulrazak Gurnah ametwaa Tuzo ya Nobel kwa upande wa Fasihi kwa mwaka 2021. Tuzo hii ya Nobel imetolewa kwa Mwanafasihi Gurnah ni kutokana na kuwa, yeye akivunja pengo kubwa kati ya utamaduni na mabara alifanya utafiti na uchunguzi kwa nia thabiti na moyo wa huruma juu ya ukoloni na hatma ya wakimbizi.

Taasisi ya Fasihi ya Sweden ilisema, utafiti usio na ukomo uliosukumwa na shauku juu ya ujuzi unaonekana kwenye vitabu vyote vilivyoandikwa na Gurnah. Na “Riwaya za Gurnah zimetusimulia hali ya Afrika Mashariki yenye utamaduni wa pande nyingi ambayo watu wengi wa sehemu nyingine duniani bado hawajaijua, na masimulizi ya mwanafasihi huyo ni yasiyotumiwa na watu wa kawaida na bila kufuata kanuni zilizowekwa.”

Taasisi hiyo ya fasihi imeongeza kuwa, Gurnah amechapisha Riwaya kumi kwa ujumla, na masimulizi mengine mafupi. Hali ya wakimbizi ni maudhui ya utunzi wa vitabu vyake vyote. Alianza kuandika riwaya alipokuwa na umri wa miaka 21 akiwa uhamishoni nchini Uingereza, ingawa Kiswahili ni lugha yake ya kwanza, lakini Kiingereza imekuwa lugha yake ya utunzi wa fasihi.

Gurnah alizaliwa mwaka 1948 na kukua kisiwani Zanzibar, alifika Uingereza kama mkimbizi mwishoni mwa miaka ya 1960. Kabla yakustaafu kwake hivi karibuni, siku zote alikuwa ni profesa wa somo la Kiingereza na somo la fasihi za baada ya ukoloni katika Chuo Kikuu cha Kent, Centerbury. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha