Huku kukiwa na hatari ya kushindwa kulipa madeni, Bunge la Marekani lafikia muafaka wa muda mfupi juu ya kuongeza kikomo cha deni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2021

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya kiongozi wa wabunge walio wengi wa Chama cha Democrats Chuck Schumer na Mitch McConnell kiongozi wa wabunge wa Republicans yataongeza kikomo cha lazima cha deni hadi kufikia dola za kimarekani Bilioni 480, kiasi ambacho kinawezesha Wizara ya Fedha ya Marekani kuweza kukidhi mahitaji ya Serikali hadi itakapofika Desemba 3, mwaka huu wa 2021, kulingana na ripoti ya Chombo cha habari cha Bloomberg ambayo ilinukuliwa pia na Shirika la Habari la Xinhua .

Kiongozi wa wabunge walio wengi wa Democrats Chuck Schumer amesema Alhamisi ya wiki hii kwamba amefikia makubaliano na wabunge wa Republicans kuhusu kuongeza kikomo cha deni la Serikali Kuu hadi Desemba mwaka huu.

“Tumefikia makubaliano kuongeza kikomo cha deni hadi Desemba, na ni matumaini yetu kwamba tunaweza kufanikisha hili mapema iwezekanavyo” Schumer alisema wakati akihutubia Bunge.

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya kiongozi wa wabunge walio wengi wa Chama cha Democrats Chuck Schumer na Mitch McConnell kiongozi wa wabunge wa Republicans yataongeza kikomo cha lazima cha deni hadi kufikia dola za kimarekani Bilioni 480, kiasi ambacho kinawezesha Wizara ya Fedha ya Marekani kuweza kukidhi mahitaji ya Serikali hadi itakapofika Decemba 3, mwaka huu, kulingana na ripoti ya Chombo cha habari cha Bloomberg ambayo ilinukuliwa pia na Shirika la Habari la Xinhua .

Makubaliano haya yanakuja wakati Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amenukuliwa mara kadhaa akionya kwamba, nchi hiyo inaweza kushindwa kulipa madeni yake kama Bunge litashindwa kupandisha au kusimamisha kikomo cha deni ifikapo Oktoba 18 mwaka huu.

“Ninaichukulia Oktoba 18 kama muda wa mwisho. Itakuwa ni hatari kutokulipa madeni ya serikali, kwetu sisi kuwa kwenye nafasi ya kukosa rasilimali za kulipa matumizi ya serikali” Yellen alinukuliwa akisema mapema wiki hii katika mahojiano na chombo cha habari cha CNBC.

Ikulu ya Washington Alhamisi hii iliyataja makubaliano ya muda mfupi juu ya kikomo cha deni ‘hatua chanya kuelekea mbele” ikiashilia Ikulu inaunga mkono makubaliano hayo.

“Na inatupa nafasi ya kupumua kutoka kwenye hatari ya kushindwa kulipa madeni tuliyokuwa tunakaribia kutokana na Seneta McConnell kucheza siasa kwenye uchumi wetu” Naibukatibu wa habari wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre aliwaambia waandishi wa habari.

“Kutatua suala la kikomo cha deni hakupaswi kuwa mpira kati ya vyama, hii ni kuhusu kulipa madeni ambayo pande zote zimehusika nayo” Jean-Pierre alisema.

Taarifa zaidi zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari zinasema, jioni ya Alhamisi ya wiki hii, Bunge la Marekani lilipitisha rasmi muswada huo wa kuongeza kikomo cha deni kwa kura 50-48

Kama sehemu ya makubaliano ya pande zote mbili juu ya Bajeti yaliyofikiwa Mwezi Agosti 2019, Bunge lilisimamisha kikomo cha deni hadi Julai 31, 2021. Baada ya kikomo cha deni kurejeshwa tena Agosti 1, 2021, Wizara ya Fedha ya Marekani ilianza kutumia ‘hatua zisizo za kawaida’ kuendelea kugharamia matumizi ya Serikali.

Kikomo cha deni, ni jumla ya kiasi cha fedha ambacho Serikali Kuu ya Marekani inaidhinishwa kukopa ili kukidhi majukumu yake ya kisheria ikiwemo usalama wa jamii na huduma za afya, riba kwenye deni la taifa na malipo mengine. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha