Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 110 ya Mapinduzi ya Mwaka 1911 Wafanyika Beijing

(CRI Online) Oktoba 09, 2021

Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 110 ya Mapinduzi ya Mwaka 1911 umefanyika leo Beijing.

Rais Xi Jinping wa China alipotoa hotuba kwenye mkutano huo alielezea tukio hilo la kihistoria lililotokea miaka 110 iliyopita linaonesha nini kwa watu wa China.

Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi amesema, historia ya mapinduzi ya mwaka 110 imetupa mwanga kuwa, ili kutimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China, lazima kuwe na nguvu kubwa ya kuwaongoza watu wa China kusonga mbele, na nguvu hiyo ndio Chama cha Kikomunisti cha China. Amesema bila ya Chama cha Kikomunisti cha China, isingekuwepo China Mpya wala ustawishaji mkubwa wa Taifa la China, akisisitiza juhudi za kuhakikisha Chama kinasimama kama uti wa mgongo wa kutegemeka kwa Taifa la China na watu wa China.

Rais Xi amesema,  miaka 110 ya mapinduzi hayo imetuambia kuwa ili kutimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China, njia inayofuata China ni muhimu sana. Ujamaa wenye umaalum wa China umethibitishwa kuwa ni njia sahihi pekee.

Ameongeza kuwa China itahakikisha utekelezaji wa Mpango wa jumla wa kusukuma mbele Maendeleo ya Sekta Tano za uchumi, siasa, utamaduni, jamii na mazingira ya asili kwa Uratibu, na kuhimiza utekelezaji wa Mkakati Kamili wa Kazi Kuu Nne kwa uwiano, kuendeleza kwa kina mageuzi na kufungua mlango kwa pande zote, kuboresha mfumo na uwezo wa kushughulikia mambo ya ndani kuwa wa kisasa, na kufanya kazi juu chini kutimiza matakwa ya watu ya kuwa na maisha bora, na kutimiza ustawi kwa wote. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha