Tazama kutoka angani: Kituo cha kitaifa cha sleji na vyombo vya kuteleza kwenye theluji cha Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021

Kituo cha sleji na vyombo vya kuteleza kwenye theluji kiko kwenye kusini magharibi mwa uwanja wa Yanqing wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022. Kimejengwa kwa kufuata sura ya Mlima mdogo wa Haituo wenye mita 2198 kutoka usawa wa bahari, na kwa jumla kina urefu wa mita 1975. Kituo hiki ni uwanja wa kipekee wa michezo ya sleji na vyombo vya kuteleza kwenye theluji nchini China, na pia ni uwanja wa 17 unaofika kigezo cha mashindano ya Michezo ya Olimpiki duniani, na wa 3 katika Asia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha