FAO yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na njaa, mabadailiko ya tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021

ROMA, (Xinhua) - Viongozi kutoka Kundi la nchi 20 (G20) wanapaswa kufanya umuhimu wao katika kukabiliana na njaa na mabadiliko ya tabianchi duniani, amesema mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Ijumaa iliyopita.

Akihutubia mkutano wa maspika wa bunge wa nchi za G20, Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu alisema FAO iko tayari kusaidia juhudi za kupambana na njaa na utapiamlo, akitaka "ushirikiano wa kina" kati ya nchi na washirika wengine wa kimataifa kama FAO.

Qu amesema, "Mkutano huu labda ni moja ya mikutano muhimu zaidi iliyoendeshwa na Italia ikiwa nchi mwenyekiti wa G20, unaleta pamoja maafisa ambao wanaweza kutunga sera na mifumo ya kisheria katika kushughulikia changamoto kubwa ambazo tunakabiliana pamoja duniani."

Alisema kuwa FAO inatambua kwamba Wabunge ni "washirika wa kimkakati kwani wanapitisha mifumo ya kisheria, wanaidhinisha ugawaji wa bajeti ya umma, na kuhakikisha uwajibikaji wa serikali juu ya ahadi za kimataifa."

Wakati Italia kuwa nchi mwenyekiti wa G20, ambao utakamilika mwaka huu, nchi wanachama wamesisitiza na kuimarisha ahadi zao za kisiasa kuhusu suala la usalama wa chakula na lishe bora duniani.

Wakati akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa G20 (B20), Qu alitaka kuboreshwa na kuimarishwa kwa mifumo yenye shirikishi zaidi ya kilimo na chakula ili kukabiliana kudidimia kwa uchumi kutokana na janga la COVID-19.

"Athari mbaya zaidi za janga la COVID-19 juu ya usalama wa chakula na lishe zimetokana na kiwango kisicho cha kawaida cha kudidimia kwa uchumi," Qu alisema, akionya kuwa "kasi isiyo sawa ya kufufuka kwa uchumi" inakuwa hatari zaidi kwa nchi mbalimbali. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha