Waziri wa mambo ya nje wa China atoa wito wa juhudi za pamoja za kuondoa ugaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021

Mjumbe wa taifa ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi tarehe 8 mwezi huu, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na kushirikiana ili kuondoa "saratani" ya ugaidi, na kuongeza kuwa China itaendelea kutoa suluhisho zake kwenye juhudi za kupambana na ugaidi duniani.

Wang alisema hayo kupitia taarifa ya maandishi kwenye Mkutano wa 11 wa mawaziri wa Baraza la kupambana na Ugaidi duniani.

Shukrani kwa juhudi za pamoja za nchi zote, maendeleo makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi. Lakini, makundi ya kigaidi bado hayajaangamizwa, mitandao bado inaendelea kukua, janga linaloendelea la UVIKO-19 limeleta ugumu zaidi katika kupambana na ugaidi, Wang amesema.

"Kupambana na ugaidi bado ni kazi kubwa kwa jumuiya ya kimataifa, na ushirikiano wa kupambana na ugaidi duniani lazima uimarishwe badala ya kudhoofishwa," Wang alisema.

Wang alitoa mapendekezo matano juu ya mapambano dhidi ya ugaidi katika siku za baadaye: kutoa uhusika kamili wa umuhimu wa Umoja wa Mataifa (UN), kuzingatia mikakati ya kushughulikia dalili na sababu kuu, kuacha kutumia vigezo viwili, kuzuia vitisho na changamoto mpya za ugaidi, na kuimarisha ujenzi wa uwezo kwa nchi zinazoendelea katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Wang alisema ugaidi ni adui wa pamoja wa binadamu. Kushughulikia tishio la mambo ya ugaidi ni kipaumbele kwa kila nchi. "Tunahitaji kutupia macho kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu, kushikamana na kushirikiana ili kuondoa 'saratani' ya ugaidi."

Akibainisha kuwa China imekuwa mshiriki na mchangiaji muhimu katika kampeni ya kimataifa dhidi ya ugaidi, Wang alisema China itaendelea kufanya mawasiliano na ushirikiano na nchi nyingine juu ya kupambana na ugaidi na watu wenye msimamo mkali na kutoa uzoefu wa China kwa dunia nzima katika mapambano dhidi ya ugaidi.  

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha