Japani yazingatia kujenga “chombo cha doria kwenye anga ya juu”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2021

Wizara ya Ulinzi ya Japani inazingatia kujenga “chombo cha doria kwenye anga ya juu” ambacho kitatumiwa katika kutoa tahadhari, kufanya ufuatiliaji, na kufanya ukarabati na kuongeza nishati kwa satlaiti kwenye anga ya juu.

Tarehe 10, Shirika la Habari la Japani lilinukuu maneno ya mhusika likisema, ikiwa sehemu moja ya kuboresha uwezo wa kufanya ufuatiliaji kwenye anga ya juu, wizara ya ulinzi ya Japan inazingatia kujenga chombo cha doria kwenye anga ya juu bila rubani, na inataka kuomba yen milioni 100 (takriban Dola za Marekani 900,000) kwa uchunguzi na utafiti katika bajeti ya mwaka 2022. Na siku ya kuanza kujenga chombo hicho bado haijaamuliwa.

Lakini, kwa kuwa kazi ya kuiwezesha chombo hicho kikaribie satelaiti inayoruka kwa kasi kwenye obiti inatakiwa kutegemea teknolojia ya hali ya juu, ofisa wa Wizara ya Ulinzi ya Japani alisema, “bado hatujajua lengo hili litaweza kutimizwa au la.”

(Hui Xiaoshuang/Tovuti ya Shirika la China Xinhua) 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha