Xining yaweka mikakati kujijenga kuwa Mji wa furaha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2021

Xining, Mji Mkuu wa Mkoa wa Qinghai Kaskazini Magharibi mwa China, umeshuhudia uboreshaji wa ikolojia ya mazingira na ustawi wa umma kutokana na juhudi za miaka kadhaa, na kuufanya kuwa moja ya miji kumi bora ambayo watu wake wana furaha zaidi nchini China. Sasa wakazi kutoka makabila mbalimbali mjini humo, ambao pia ni mji mkubwa katika Bonde la Qinghai-Tibetan, wanaishi kwa amani na furaha.

Picha inayoonesha eneo la bustani huko Xining, Mji wa Mkoa wa Qinghai uliopo Kaskazini Magharibi mwa China. (Tovuti ya Gazeti la Umma / Yang Qian)

Mji umeweka kipaumbele katika uhifadhi wa ikolojia na maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, na kuleta mazingira mazuri ya kuishi kwa wakazi wake katika miaka ya hivi karibuni. Juhudi hizi zimeongeza kiwango cha msitu hadi asilimia 36 na zimeongeza kiwango cha ukubwa wa bustani kwa kila mtu kutoka mita za mraba 12 hadi 13. Kwa msisitizo zaidi, ukubwa wa msitu wa milima ya Nanshan na Beishan umeongezeka kutoka asilimia 7.2 hadi asilimia 79, ambayo imeongeza sana kiwango cha hewa ya oksijeni ya eneo hilo huku ikipunguza uwezekano wa majanga ya kijiolojia kama maporomoko ya ardhi na maporomoko ya matope.

Kutokana na kuboreshwa kwa mazingira yake, Xining imejitahidi kukuza sekta yake ya utalii, ambayo imeleta faida kubwa kwa wakazi. Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa rasmi, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2021, mji huo ulipokea zaidi ya watalii milioni 10.3, likiwa ni ongezeko la asilimia 66.81 kuliko mwaka jana, na mapato ya utalii yamefikia Yuan bilioni 10.8 (karibu dola za kimarekani bilioni 1.67), sawa na asilimia 94.31 kuliko mwaka uliopita wa 2020 wakati kama huo.

Picha ikionesha mandhari ya "bahari ya maua" katika kijiji cha Bianmagou huko Xining, Mkoa wa Qinghai uliopo Kaskazini Magharibi mwa China. (Tovuti ya Gazeti la Umma/ Yang Qian)

Kwa mfano, kijiji cha Bianmagou kilichopo katika Kaunti inayojiendesha ya kabila la WaHui na kabila la WaTu ya Datong kimeendeleza utalii wa vijijini kwa kutumia maliasili ya maumbile na mpango wa China wa kupunguza umaskini.

Katika siku za nyuma, mazao yanayopatikana katika ardhi ndogo hayawezi kukidhi mahitaji ya familia kutokana na ardhi isiyokuwa na rutuba, kwa hivyo vijana waliondoka eneo hilo kutafuta kazi mahali pengine. Mnamo mwaka wa 2016, eneo la "bahari ya maua" katika kijiji hicho lilifunguliwa kwa ajili ya utalii, ambalo limesaidia wakazi kufurahia maisha bora.

Eneo hilo lenye mandhari ya kupendeza lilivutia watalii 300,000 katika mwaka wa kwanza wa kufunguliwa kwake, hivyo kuwasaidia wanakijiji wote kuondolewa umaskini katika eneo hilo. Mwaka jana, eneo hilo lilipokea zaidi ya watalii 800,000, na mauzo ya tiketi yalifikia Yuan milioni 4.5 na thamani ya biashara ya hoteli za karibu na maduka yakifikia Yuan milioni 15. Uwiano wa mapato kwa kila mwanakijiji uliongezeka hadi yuan 18,450 katika Mwaka 2020 kutoka Yuan 1,800 ya mwaka 2015.

Picha ikionesha kituo cha utoaji elimu wa uzalendo katika kijiji cha Xiaogaoling huko Xining, Mkoa wa Qinghai Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha kutoka Tovuti ya Gazeti Umma/ Xie Ying)

Tie Chengyu, mwenye umri wa miaka 57, ni mmoja wa wenyeji ambao wamefaidika na maendeleo ya utalii wa vijijini kwa kuendesha mgahawa vijijini. Mwaka jana, Tie alipata mapato yanayofikia yuan 100,000 kutoka kwenye mgahawa huo, kwa kupokea ada ya kukodisha shamba lake ambalo limebadilishwa kuwa eneo la kitalii, pia bonasi ya kila mwaka ya mapato ya utalii ambayo hugawanywa kwa wanakijiji na mamlaka ya kijiji hicho. Tie ana mipango ya kujenga nyumba yenye ghorofa mbili ili kuendesha biashara yake ya mgahawa katika siku zijazo pamoja na mtoto wake.

Aidha, Xining imeanza kuendesha sekta yenye umaalum. Mazulia ya kitibet ni moja ya kazi za ubunifu wa asili zinazofanyika kwenye Bonde la Qinghai-Tibetan. Mwaka 2006, stadi za kufuma mazulia ya kitibet ya kijiji cha Jiaya ziliorodheshwa katika orodha ya kwanza ya kitamaduni usiyoshikika wa China.

Picha ikionesha zulia la kitibet lililotengenezwa na Kampuni ya Shengyuan Carpet Group Co, Ltd, kampuni ya kutengeneza mazulia ya kitibet iliyoko Xining, huko Qinghai Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha Kutoka Tovuti ya Gazeti la Umma/Yang Qian)

Kampuni ya mazulia ya Shengyuan ni kampuni ya kutengeneza mazulia ya kitibet iliyoko Xining. Kwa kujumuisha teknolojia ya hali ya juu katika ustadi wa jadi wa kutengeneza mazulia, kampuni hiyo imeboresha kiwango cha ustadi wa jadi wa mazulia. Imesafirisha bidhaa zake kwa nchi na sehemu zaidi ya 40, na thamani ya pato la kila mwaka linakadiriwa kufikia yuan milioni 80.

Rais Xi Jinping wa China alipotembelea kampuni hiyo wakati amefanya ziara katika Mkoa wa Qinghai Mwezi Juni mwaka huu alisema, uzalishaji wa mazulia ya kitibet ni shughuli ya kiuchumi inayoendana na hali halisi ya Qinghai, na inasaidia watu kuondolewa umaskini, kustawisha maisha ya watu vijijini na kuimarisha mshikamano wa makabila yote yanayoishi eneo hilo.

Picha ikionesha Kituo cha kiraia cha Xining huko Xining, Mji Mkuu wa Mkoa wa Qinghai ulioko Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha Kutoka Tovuti ya Gazeti la Umma/ Xie Ying)

Zaidi, Xining imetoa kipaumbele katika kuboresha huduma za umma. Kituo cha kiraia cha Xining, mradi muhimu wa kuhakikisha ustawi wa watu katika mkoa huo, kinawezesha wakazi na wafanyabiashara kupata huduma za serikali katika eneo moja na kutoa huduma za kawaida.

Hadi sasa, idara 36 za serikali zimetoa huduma za aina 500 ya kiserikali katika kituo hicho.

Mji wa Xining umeimarisha juhudi za kuboresha huduma za jamii na kuimarisha mshikamano wa makabila mbalimbali ya eneo hilo. Jamii ya Wentingxiang, ambayo wanaishi zaidi ya wakazi 22,769 kutoka makabila mbalimbali, hufanya shughuli mbalimbali kama vile kupika pamoja kusherehekea sikukuu za jadi na kuoneshana picha za zamani ili kuongeza hali ya furaha miongoni mwao. Jamii hiyo pia hutoa huduma kwa watoto baada ya shule na huduma za nyumbani kwa wazee.

Picha ya pamoja ya Gao Shuzhen na mjukuu wake kutoka jamii ya Wentingxiang huko Xining, Mji Mkuu wa Mkoa wa Qinghai Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha Kutoka Tovuti ya Gazeti la Umma/Yang Qian)

Gao Shuzhen, mwenye umri wa miaka 65, anafurahia maisha yake sasa katika jamii hiyo. "Shughuli zetu za kijamii mara nyingi huwavutia jamaa na marafiki mara ninapoziweka kwenye mitandao ya kijamii," Gao alimwambia Mwandishi wa Tovuti ya Gazeti la Umma.

 "Serikali imejali kila upande wa maisha ya wakazi, na ninajisikia furaha kuishi Xining," Gao alisema kuhusu maisha yake, akielezea kuwa pensheni yake ya kustaafu inaongezeka kila mwaka na anafurahia kiwango cha juu cha ulipaji wa bima ya matibabu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha