Rais wa Tanzania apenda kuhimiza uhusiano kati ya Tanzania na China uendelezwe kwenye kiwango kipya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2021

Tarehe 11, rais Samia wa Tanzania alisema, urafiki wa Tanzania na China ulianzishwa na viongozi waasisi wa nchi hizo mbili. Tanzania ingependa kuendelea kushirikiana na China katika kuhimiza pamoja uhusiano kati ya nchi hizo mbili uendelezwe kwenye kiwango kipya.

Siku hiyo huko Dodoma, rais Samia alipopokea nyaraka za Utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China, Bi. Chen Mingjian alisema, anashukuru msaada mkubwa usio na ubinafsi kutoka kwa serikali ya China na watu wake katika maendeleo na ujenzi wa nchi ya Tanzania.

Bi. Chen Mingjian alisema, urafiki wa jadi wa China na Tanzania ni mkubwa sana, na umejaribiwa katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko mengi duniani. Katika miaka ya karibuni iliyopita, hali ya kuaminiana ya kisiasa ya nchi hizo mbili inaendelea kuimarishwa, pande hizo mbili zinaungana mkono juu ya mambo yanayohusu maslahi makuu ya kila upande, na zimepata matunda mengi kwenye ushirikiano wa sekta mbalimbali. China ingependa kuimarisha urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati yake na Tanzania katika sekta mbalimbali, kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande zote kati ya China na Tanzania, ili kuleta manufaa kwa nchi hizo mbili na watu wao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha