Watu watano wauawa Somalia katika mlipuko wa kujitoa muhanga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2021

MOGADISHU—Angalau watu watano wamefariki na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga lililotokea katika Mji Mkuu wa Somalia Mogadishu Jumanne jioni, polisi na mashuhuda wamesema.

Afisa wa polisi ambaye amekataa kutajwa jina lake, ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwamba mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliingia kwenye mkahawa karibu na makutano ya Fagah na kujilipua, na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kadhaa kujeruhiwa.

"Tunaweza kuthibitisha kuwa watu watano wamefariki katika mlipuko huo na wengine wamejeruhiwa," alisema.

Mashuhuda wamesema walisikia mlipuko mkubwa katika makutano ya Fagah mjini Mogadishu.

  "Mlipuko ulikuwa mkubwa na nimeona watu waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini," alisema Abdirahman Mohamed, shuhuda wa tukio hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha