UNICEF yaonesha wasiwasi juu ya usalama wa watoto wahamiaji katika vituo vya kizuizi vya Libya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2021

TRIPOLI, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) Jumanne ya wiki hii limeeleza wasiwasi wake juu ya usalama wa watoto wahamiaji wanaoshikiliwa katika vituo vya kizuizi katika Mji Mkuu wa Libya Tripoli.

Taarifa ya UNICEF inasema, usalama na maslahi ya wanawake na watoto wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watano wasio na walezi na watoto wachanga wasiopungua 30 wanaoshikiliwa katika vituo vya kizuizi huko Tripoli, unakabiliana na hatarini.

Karibu wanawake 751 na watoto 255 kati ya maelfu ya wahamiaji na watafuta hifadhi walikamatwa katika operesheni iliyotekelezwa na Libya hivi karibuni mjini Tripoli, UNICEF imesema.

"Wahamiaji na watoto wakimbizi nchini Libya wanaendelea kukabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto ikiwa ni pamoja na kuwekwa kizuizini," alisema Cristina Brugiolo, Kaimu mjumbe maalum wa UNICEF nchini Libya.

UNICEF na washirika wengine wa kutoa huduma za kibinadamu wamehimiza mamlaka za Libya kuwalinda watoto na kuzuia kutengana kwao na wazazi wao, walezi wao, na familia.

UNICEF pia ilitaka kuachiliwa mara moja kwa watoto wote katika vituo vya kizuizi kote Libya.

"UNICEF pamoja na washirika wake iko tayari kutoa msaada wa kiufundi pamoja na mipango mbadala ya utunzaji wa watoto waliowekwa kizuizini," alisema Brugiolo.

Libya imekuwa ikikumbwa na ukosefu wa usalama na machafuko tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi Mwaka 2011, na kuifanya nchi hiyo kuwa mahali yanayokuja kwa wengi wahamiaji haramu ambao wanataka kuvuka Bahari ya Mediterania kwenda pwani za Ulaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha