Rais Xi atoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya usafirishaji, maendeleo ya pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2021

(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping wa China Alhamisi wiki hii ametoa wito wa kuendeleza ushirikiano wa usafirishaji wa kimataifa na kukuza maendeleo ya pamoja wakati wa mabadiliko ya dunia na janga la UVIKO-19.

Akihutubia kupitia njia ya video katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Usafirishaji Endelevu wa Umoja wa Mataifa Jijini Beijing, Xi alitoa wito wa "kuandika ukurasa mpya unaojumuisha muunganiko wa miundombinu, biashara na uwekezaji zisizo na vizuizi, na maingiliano ya ustaarabu wa Dunia".

Mkutano huo, uliopangwa kufanika kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi wiki hii, utatilia mkazo umuhimu wa usafirishaji endelevu katika kufanikisha Ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu. Zaidi ya wawakilishi 171 kutoka nchi mbalimbali wanahudhuria mkutano huo mtandaoni na nje ya mtandao.

Huku akisisitiza kuwa, usafirishaji ni moyo wa uchumi na mapatano kati ya ustaarabu, Xi amesema usafirishaji umehimiza utandawazi wa uchumi na mawasiliano ya watu, na kugeuza dunia kuwa kijiji kilichounganishwa kwa karibu.

"Ni kupitia kufungua mlango, kuwa na masikiliano na muunganiko tu, nchi zinaweza kuimarisha juhudi za pamoja na kunufaishana" Xi amesema.

Ametoa wito wa maingiliano ya kina kati ya teknolojia mpya kama vile takwimu kubwa, mtandao wa Internet, akili bandia na mfumo ya akiba ya data ya kidijitali na sekta ya uchukuzi, na kufanya juhudi zaidi za kukuza uchukuzi unaotoa Carbon chache.

Rais Xi ametangaza kuwa, China itaanzisha Kituo cha kimataifa cha Uvumbuzi na Ujuzi kuhusu Usafirishaji Endelevu, na kutoa mchango wake katika maendeleo ya usafirishaji duniani.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitaka nchi zote duniani kushirikiana ili kujenga mifumo endelevu zaidi ya usafirishaji na kuharakisha mchakato sekta ya uchukuzi kutimiza lengo la utoaji chache wa Carbon.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha