Maafisa wa Xinjiang na wakulima wa pamba wakanusha uwongo wa "kulazimishwa kufanya kazi"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2021

URUMQI - Kaunti ya Xayar iliyopo Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China mwishoni mwa wiki hii imefanya mkutano na waandishi wa habari ambapo wakulima wa pamba na maafisa wa eneo hilo wamekanusha vikali uwongo wa "kulazimishwa kufanya kazi" huko Xinjiang ambao umetungwa na kuenezwa na watu wasiyoipenda China kutoka nchi za Magharibi.

Kwa mujibu wa Afisa wa Wilaya ya Aksu, Niyaz Axim, Aksu ni moja ya maeneo makubwa zaidi ya uzalishaji wa pamba huko Xinjiang, lenyehekta 500,000 ya ardhi ya upandaji wa pamba. Uzalishaji pamba katika eneo hilo linachukua zaidi ya asilimia 90 ya jumla ya uzalishaji wa pamba kote nchini China.

Mnamo mwaka 2020, sekta ya utengenezaji nguo na mavazi huko Aksu ilitoa ajira 102,000, ikiwapatia wafanyakazi mapato ya wastani wa yuan 3,600 hadi 5,000 (sawa na dola za kimarekani 559 hadi 777) kila mwezi.

Niyaz Axim amesema, idara za serikali za mitaa zinalinda kikamilifu haki za wafanyakazi katika sekta ya uzalishaji pamba, na wafanyabiashara wa nguo na mavazi husaini mikataba ya kazi na wafanyakazi kulingana na sheria.

Ameongeza kuwa, makabila yote hupokea malipo sawa kwa kazi sawa, pia wanafurahia bima ya jamii, mafunzo, muda wa likizo na haki zingine halali za kikazi. Kampuni hizo zinaheshimu kikamilifu imani za kidini, mila, lugha na haki zingine za wafanyakazi kutoka jamii za makabila madogo.

Muhtar Rohman, mkulima wa pamba, amekuwa dereva wa mashine ya kuokota pamba tangu miaka miwili iliyopita. Amesema anaweza kupata zaidi ya Yuan 100,000 kila mwaka. Kwa sasa anamfundisha kaka yake na watu wengine mbinu za ukarabati wa mashine na jinsi ya kuendesha mashine za kuokota pamba na matrekta. "Ninaamini kuwa watakapokuwa na ujuzi, watapata pesa zaidi kama mimi," amesema.

 "Niliona mitandaoni baadhi ya watu wanaoichukia China wakiituhumu Xinjiang juu ya ‘kulazimishwa kufanya kazi' kwenye mashamba ya uzalishaji pamba, kitu ambacho ni uongo wa wazi" amesema Muhtar Rohman. "Ninategemea teknolojia na bidii kupata pesa, inawezaje kuwa 'kulazimishwa kufanya kazi’?"

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha