Kijana Shi Yilong: Kushikilia kufanya kwa unavyopenda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2021

Akiwa na umri wa miaka 28, Bw. Shi Yilong aliwahi kuwa mchezaji aliyenyakua ubingwa wa michezo ya kimataifa, alikuwa mwongozaji wa filamu, alianzisha shughuli zake, na alikuwa dereva wa teksi. Lakini sasa amekuwa nyota wa michezo mtandaoni mwenye mashabiki zaidi ya milioni 2.

Akina vijana kama Shi Yilong huitwa kuwa "vijana waasi" yaani vijana wanaokiuka desturi na kanuni zilizowekwa, lakini kwa Shi, neno "mwasi" lina maana nzuri, linamaanisha watu wanashikilia kufanya kwa wanavyopenda, na pia ni mchakato wa kujitambulisha tena na tena. Alisema "ninapenda kushindana na mimi mwenyewe."

Hivi sasa machoni mwa marafiki zake, Shi ni mtu anayefaulu kwa "kucheza ubao wa kutekeleza"— Sasa ana kampuni yake mwenyewe. Shi alisema, "Ukifanya jambo moja kwa makini kwa miaka 10 mfululizo, bila shaka utapata matunda. Mimi nilifanya vivyo hivyo. Nimefanya mambo ninayopenda kwa miaka mingi, na nimebadilika kuwa mtu mwenye kampuni kutoka mtu asiye na pesa hata kidogo. Mafanikio hayo yote yanatokana na ushabiki wangu."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha