Pato la Taifa la China lakua kwa asilimia 9.8 katika robo tatu za kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2021
Pato la Taifa la China lakua kwa asilimia 9.8 katika robo tatu za kwanza
Picha iliyopigwa mnamo Julai 13, 2021 ikionesha kituo cha kupokea na kusafirisha makontena huko Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang Mashariki mwa China. (Xinhua / Long Wei)

BEIJING - Uchumi wa China umeendelea kuimarika katika robo tatu za kwanza za mwaka huu huku viashiria muhimu vikidumu katika kiwango sahihi, takwimu rasmi zilionesha Jumatatu ya wiki hii.

Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zimeonesha kuwa, pato la taifa la nchi hiyo (GDP) limekua kwa asilimia 9.8 katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, na kufanya wastani wa ukuaji kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwa asilimia 5.2.

Katika robo ya tatu (Q3), Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 4.9, ikiwa ni ongezeko ndogo kuliko asilimia 18.3 katika robo ya kwanza (Q1) na asilimia 7.9 katika robo ya pili (Q2).

"Uchumi wa China umedumisha kasi ya kufufuka katika robo tatu za kwanza huku kukiwa na maendeleo katika maboresho ya kimuundo na maendeleo ya kiwango cha juu," Msemaji wa NBS Fu Linghui.

Kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kimebaki kuwa asilimia 4.9 mnamo Septemba, ikiwa ni kiwango cha chini kwa asilimia 0.5 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, takwimu za NBS zimeonesha. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha