China yatoa mwongozo kuhusu uchumi wa kijani mijini na vijijini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2021

Beijing - Ofisi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na ofisi ya Baraza la Serikali la China zimetoa mwongozo unaoelekeza maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya mijini na vijijini.

Mwongozo huo unaweka lengo kwamba ifikapo mwaka 2025 taratibu za kitaasisi na mifumo ya sera za maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya mijini na vijijini itaanzishwa.

Unaeleza kwamba, China pia itapata maendeleo makubwa katika kubadilisha muundo wa uchumi wa kijani na kuendeleza kikamilifu upunguzaji wa utoaji wa kaboni katika kipindi hicho.

Mwongozo unasisitiza kuwa, matukio ya "magonjwa ya mijini" yanapaswa kupunguzwa, ubora wa ikolojia na mazingira ya asili utaboreshwa na mtindo wa maisha usiyoleta uchafuzi kwa mazingira utaenezwa zaidi.

Mwongozo unaweka lengo lingine kuwa ifikapo mwaka 2035 maendeleo ya uchumi wa kijani yatahusisha kwa pande zote maeneo ya mijini na vijijini, pamoja na kupungua kwa utoaji wa kaboni.

Ifikapo muda wa kufikia lengo hilo, mazingira ya kuishi yataboreka na mfumo na uwezo wa kimsingi wa usimamizi utakuwa wa kisasa katika ujenzi wa mijini na vijijini.

Kama sehemu ya kukuza maendeleo ya pamoja ya mijini na vijijini, mwongozo huo unasisitiza maendeleo ya uchumi wa kijani ya mikoa mbalimbali na makundi ya miji, na kuahidi kujenga miji mizuri yenye masikilizano kati ya binadamu na viumbe asili na vijiji vizuri vyenye maendeleo yasiyochafua mazingira, mazingra mazuri ya asili na yanayofaa maisha ya binadamu.

Aidha, mwongozo huo unatoa wito wa kuboreshwa kwa mifumo ya maendeleo inayohusisha ujenzi wa kiwango cha juu unaozingatia uhifadhi wa mazingira na miundombinu bora katika maeneo ya vijijini na mijini.

Mwongozo unaeleza zaidi kwamba, nchi inapaswa kuimarisha uhifadhi na urithi wa historia na utamaduni katika miji na maeneo ya vijijini, kuzingatia ujenzi usiyoharibu mazingira na kukuza ujenzi wa mtindo wa maisha yasiyochafua mazingira.

Mwongozo huo pia unasema, China pia inapaswa kuratibu mipango na ujenzi wa miji na maeneo ya vijijini, kuanzisha mfumo wa tathmini, kuzidisha uvumbuzi wakati wa mchakato huo na kuhimiza ujenzi wa miji yenye mambo ya kisasa.

Mwongozo huo unaahidi kuongeza bajeti, kuboresha mfumo wa kifedha wa uchumi wa kijani, na kutoa msaada zaidi kwa miradi mikubwa ya maendeleo inayozingatia uhifadhi wa mazingira mijini na vijijini. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha