Lugha Nyingine
Xi Jinping Atoa Hotuba Kwenye Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 50 Tangu China Iliporudisha Kiti Chake Halali Kwenye Umoja wa Mataifa
Oktoba 25 hapa Beijing, Rais Xi Jinping amehudhuria Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 50 Tangu China iliporudisha kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa akitoa hotuba muhimu .
Rais Xi amedhihirisha kuwa, China Mpya ilirudisha kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa lilikuwa tukio kubwa katika dunia, pia lilikuwa ni tukio kubwa la Umoja wa Mataifa. Hayo ni matokeo ya juhudi zilizofanywa pamoja na nchi zote duniani zinazopenda amani na kutetea haki, tukio hilo lilionesha kuwa Watu wa China wanaochukua robo moja ya idadi ya watu wa dunia walikuwa wamepanda tena kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa. Tukio hilo lina umuhimu mkubwa na wa mbali kwa China na Dunia.
Rais Xi amesisitiza kuwa, miaka 50 hiyo iliyopita tangu China mpya iliporudisha kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa, ni miaka 50 kwa China kujiendeleza kwa amani, pia ni miaka 50 kwa China kuleta manufaa kwa binadamu. China itashikilia kufuata njia ya kujipatia maendeleo kwa amani, itakuwa mjenzi wa amani ya dunia siku zote; itafuata kithabiti njia ya mageuzi na kufungua mlango, itatoa mchango kwa maendeleo ya dunia nzima siku zote; itafuata njia ya kufanya ushirikiano na pande mbalimbali, na siku zote itakuwa mlinzi wa utaratibu wa kimataifa. China ingependa kujiunga na nchi mbalimbali katika kufanya mashauriano na kujenga pamoja wazo la kunufaika pamoja, kutukuza thamani ya pamoja ya binadamu wote, kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi ulio wa kweli, kusimama kwenye upande wa usahihi wa kihistoria, kusimama kwenye upande wa maendeleo ya binadamu, kufanya mapambano bila kulegalega kwa ajili ya kutimiza amani na maendeleo ya dunia ya kudumu, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Magaifa Bw. Gutres alipotoa risala alisema, katika miaka 50 iliyopita tangu China irudi kwenye Umoja wa Mataifa, China imetoa mchango mkubwa siku hadi siku, nayo ni mwezi wa kutegemeka kwa Umoja wa Mataifa na ni nguzo katikati ya ushirikiano wa kimataifa. Ameishukuru China kwa kazi yake muhimu kwa ajili ya kutimiza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na katika kuondoa umaskini, kutumia nishati safi na kupunguza utoaji wa cabon ili kulinda mazingira ya asili. Amesema, Umoja wa Mataifa utatoa uungaji mkono kwa ajili ya kutekeleza pendekezo la maendeleo ya dunia nzima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma