

Lugha Nyingine
Maonesho ya kimataifa ya Maendeleo yasiyo na uchafuzi kwa mazingira 2021 yafanyika huko Changsha, Hunan
Mkutano wa miji iliyoko kwenye eneo la kati la mtiririko wa Mto Changjiang 2021 kuhusu kufikia utoaji mdogo zaidi wa carbon na uwiano wa carbon, na Maonesho ya kimataifa ya maendeleo yasiyo na uchafuzi kwa mazingira yanafanyika huko Changsha, Hunan. (Picha/Jiangling)
Kuanzia tarehe 22 hadi 24, Oktoba, Mkutano wa miji iliyoko kwenye eneo la kati la mtiririko wa Mto Changjiang 2021 kuhusu kufikia utoaji mdogo zaidi wa kaboni na kufikia uwiano wa kaboni, na Maonesho ya kimataifa ya maendeleo yasiyo na uchafuzi kwa mazingira yanafanyika huko Changsha, mkoa wa Hunan, China. Kaulimbiu ya Mkutano huo ni “Utoaji mdogo wa Kaboni, uchumi wa mzunguko na maendeleo”. Mkutano huo unafuata mawimbi ya maendeleo ya zama za hivi sasa, na mwelekeo mkuu wa maendeleo ya sekta, na umetoa jukwaa muhimu kwa kuonesha teknolojia mpya zaidi na matunda yake ya sekta hiyo, na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano nchini na wa kimataifa.
Maonesho hayo yamepangiwa kwenye maeneo makuu manne, yaani eneo la nishati mpya na utoaji mdogo wa kaboni, eneo la sekta za viwanda za kulinda mazingira, eneo la uchumi wa mzunguko, na eneo la kubana matumizi ya nishati. Maeneo ya maonesho hayo ni mita za mraba 40,000, na yanaweka mkazo katika kuonesha kazi ya kuzuia na kushughulikia uchafuzi wa maji, hewa na udongo, kushughulikia takataka, kuonesha uchumi wa mzunguko wa kilimo na viwanda, na teknolojia na zana na vifaa husika.
Mkutano na maonesho hayo yameandaa vizuri shughuli zaidi ya 10 zinazohusisha jukwaa la mawasiliano na ushirikiano la sekta ya kubana matumizi ya nishati bila ya uchafuzi kwa mazingira, maonesho, mazungumzo ya biashara, ushirikiano kwenye miradi na kutangaza mafanikio.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma