Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing mwaka 2022 yachapisha kitabu cha kwanza cha mwongozo dhidi ya UVIKO-19

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2021

BEIJING – Toleo la kwanza la Kitabu kinachoelezea hatua za kupambana na UVIKO-19 kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing mwaka 2022 kimetolewa leo Jumatatu.

Kitabu hicho cha mwongozo, kilichochapishwa kwa pamoja na waandaaji wa Beijing 2022, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) kinatoa matoleo tofauti kwa wanariadha na maafisa wa timu pamoja na wahusika wengine ikiwa ni pamoja na familia ya wanariadha, vyombo vya habari, Mashirikisho ya Kimataifa (IFs) na maafisa wa kiufundi.

Baada ya kitabu cha mwongozo wa kudhibiti UVIKO-19 kutolewa, mfumo wa usimamizi wa kitanzi cha kufungwa utatekelezwa wakati washiriki wa michezo huo watakapokaa nchini China.

Huang Chun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kuzuia na Kudhibiti janga la UVIKO-19 katika Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 (BOCOG) amesema, washiriki wanaweza kutembelea kwa uhuru ndani ya eneo hilo la kitanzi cha kufungwa, kusafiri kwa magari maalum kati ya viwanja vya michezo na maeneo ya malazi, na kati ya maeneo matatu ya michezo hiyo za Beijing, Yanqing na Zhangjiakou.

Naibu mkurugenzi wa ofisi ya afya ya umma ya idara ya huduma za michezo ya kamati ya BOCOG Wang Quanyi amesema, China itachukua hatua kadhaa ili kutoa mazingira mazuri ya michezo hiyo. Kwa mfano, washiriki hawatalazimika kusubiri kwenye uwanja wa ndege ili kupata matokeo yao ya vipimo vya UVIKO-19 watakapowasili. Badala yake, watapelekwa hadi kwenye makazi yao na kusubiri matokeo wakiwa vyumbani.

Mfumo huo wa usimamizi wa kitanzi cha kufungwa katika eneo la michezo ya olimpiki, utaruhusu pia washiriki wa michezo ambao wameshadungwa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kuingia China pasipo kulazimika kukaa karantini na kwa yeyote ambaye atakuwa hajadungwa chanjo atalazimika kukaa karantini kwa siku 21 atakapowasili Beijing. “Jambo la pekee linaweza kuwepo kwa wale wenye sababu maalum za kiafya” kitabu hicho kinasomeka.

Toleo la pili la kitabu cha mwongozo wa hatua za kudhibiti UVIKO-19 katika michezo hiyo litatolewa Desemba mwaka huu wa 2021. "Kitabu cha toleo la kwanza la mwongozo wa jumla, kitarekebishwa katika siku zijazo" Wang amesema, "Kanuni za kina kwa kila eneo la michezo na hoteli zitawekwa kulingana na hali halisi" ameongeza.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha