Ripoti yaonesha zaidi ya asilimia 80 ya nchi na sehemu duniani zapokea uwekezaji kutoka China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2021
Ripoti yaonesha zaidi ya asilimia 80 ya nchi na sehemu duniani zapokea uwekezaji kutoka China
Picha iliyopigwa Januari 16, 2019 ikionesha Bandari ya Piraeus nchini Ugiriki.

Kampuni ya Junhe Pumps Holding Co., Ltd. yenye makao makuu yake mjini Ningbo, mkoa wa Zhejiang Mashariki mwa China imefungua matawi mawili ya kampuni yake huko Amerika Kaskazini na Ulaya katika miaka miwili iliyopita ili kukidhi mahitaji ya wateja wa wenyeji kwa bidhaa zinazoweza kukidhi matakwa yao ipasavyo.

“Tunapofanya uwekezaji zaidi katika nchi za nje, tunajawa na imani ya kuanzisha miradi mipya” Zhang Junbo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo amesema.

"Biashara yetu imeongezeka kwa asilimia 16.7 kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita huko Amerika Kaskazini. Pia tulijenga viwanda vya kidijitali ili kuongeza thamani ya bidhaa zetu” Zhang amesema huku akiongeza kuwa bidhaa zao hazijakidhi tu mahitaji ya wateja wa kigeni bali pia ni dalili ya mwelekeo mpana wa sekta hiyo.

Shauku inayoonekana kwa makampuni ya China kuwekeza katika nchi za nje umethibitisha kupanda kwa ubora na kiasi cha uwekezaji wa China katika nchi za nje. Kwa mujibu wa takwimu iliyotolewa na serikali mapema mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi za nje (ODI) ulipanda kwa asilimia 12.3 kila mwaka na kufikia dola za kimarekani bilioni 153.71 mwaka 2020, huku kiwango cha uwekezaji huo kikishika nafasi ya kwanza duniani kwa mara ya kwanza.

Uwekezaji wa China katika maeneo mbalimbali duniani ulichangia zaidi ya asilimia 10 ya uwekezaji wa dunia kwa miaka mitano mfululizo, na kufikia asilimia 20.2 ya jumla ya uwekezaji kote duniani mwaka 2020. Ripoti hiyo inaonesha zaidi kwamba, hisa za uwekezaji wa nje wa China zilifikia dola za kimarekani trilioni 2.58 na kuchukua nafasi ya tatu kati ya wawekezaji wakubwa katika soko la kimataifa hadi mwishoni mwa Mwaka 2020.

Mwaka jana 2020, uwekezaji wa China katika nchi za nje ulienda zaidi katika sekta 18, na karibu asilimia 70 yake ilienda kwenye huduma za kukodisha na biashara, utengenezaji, biashara ya rejareja na wa jumla, na sekta za kifedha. Thamani ya uwekezaji katika sekta hizi nne ilizidi dola za kimarekani bilioni 10.

"Viashiria vingi vilivyotajwa kwenye taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na faida ya mitaji yaliyowekezwa tena yalisalia katika kiwango cha juu, na ukweli kwamba kiwango cha uwekezaji kutoka kwa sekta ya uchumi usiomilikiwa na umma ilizidi sekta ya uchumi unaomilikiwa na umma, zote zilionesha makampuni ya biashara ya China yamepiga hatua kubwa katika kushiriki kwenye mnyororo wa thamani wa kimataifa na kwamba ushindani wao wa kimataifa na uwezo wao wa kufanya uwekezaji umeboreshwa kwa madhubuti,” amesema Ge Shunqi, mtafiti wa uwekezaji wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Nankai.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, zaidi ya asilimia 80 ya nchi na sehemu duniani zilikuwa zimepokea aina fulani ya uwekezaji kutoka China, huku makampuni 28,000 ya China yameanzisha makampuni 45,000 katika nchi na sehemu 189 duniani kote.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha