

Lugha Nyingine
Kufungua ukurasa mpya: Chuo Kikuu cha Cambridge na Makumbusho ya Ufaransa yarudisha mabaki ya kale ya Utamaduni kwa nchi za Afrika Magharibi
Tarehe 26, Oktoba huko Paris, kabla kufanyika kwa hafla ya kukabidhi sanaa 26 kwa Jamhuri ya Beinin, kinyago cha hadhi ya kiti chenye hadhi katika Dola ya kifalme ya Benin (karne ya 18 hadi 19) kikioneshwa kwenye Maonesho ya Jumba la Makumbusho ya Quai Branly ya Ufaransa. (Picha inatoka IC Photo.)
Taasisi ya Masomo ya Yesu ya Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza na Makumbusho ya Quai Branly ya Ufaransa yamerudisha nchini Nigeria na Jamhuri ya Benin baadhi ya mabaki ya kale ya utamaduni vilivyonyang'anywa wakati wa kipindi cha ukoloni. Hafla ya kukabidhi vinyago hivyo ilifanyika Oktoba 27, 2021. Shirika la Habari la Reuters limesema, taasisi hizo mbili zimefungua ukurasa mpya wa kurudisha mabaki ya kale ya utamaduni ya Afrika, na zitaweka shinikizo kwa taasisi na mashirika mengine katika nchi za Magharibi kurejesha mabaki ya kale ya utamaduni yaliyonyang’anywa .
Taasisi ya kwanza ya Uingereza kuchukua hatua ya kurejesha mabaki ya kale ya Afrika yaliyonyang’anywa wakati wa Ukoloni
Taasisi ya Masomo ya Yesu ya Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza ilifanya hafla ya kukabidhi kinyago cha jogoo cha zama ya Dola ya Kifalme ya Benin kwa ujumbe wa Serikali ya Nigeria Oktoba 27, 2021. Hafla hiyo ilifanyika katika chuo hicho huko London, Uingereza.
Serikali ya Nigeria imekishukuru Chuo hicho kwa kufungua ukurasa wa kurudisha mabaki ya kale ya utamaduni.
Mwaka 1897, Jeshi la Uingereza lilivamia na kukalia kimabavu dola ya kale ya Kifalme ya Benin ya Magharibi mwa Afrika, ambapo lilinyang’'anya mamia ya vyombo vya shaba nyeusi, kikiwemo kinyago hicho cha jogoo. Dola ya kale ya kifalme ya Benin ilikuwepo katika eneo la nchi ya Nigeria ya sasa.
Vyombo vya shaba nyeusi vya kipindi cha Dola ya kifalme ya Beijing ni moja ya mabaki ya kale ya utamaduni yenye umuhimu na thamani kubwa zaidi barani Afrika, na hivi sasa vingi vinahifadhiwa kwenye majumba ya makumbusho na taasisi nyingi za nchi za Ulaya na Marekani. Na vyombo hivyo vinavyohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Uingereza ni vingi zaidi kuliko mashirika mengine.
Rais wa Ufaransa aendesha hafla ya makabidhiano
Mjini Paris, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliendesha hafla iliyofanyika kwenye Jumba la Makumbusho la Quai Branly ya kurudisha mabaki ya kale 26 ya utamaduni kwa upande wa Benin, ambayo yalinyang’anywa na Jeshi la Ufaransa mwaka 1892 kutoka dola ya kale ya kifalme ya Beinin.
Mtaalam mmoja wa historia ya sanaa wa Ufaransa amesema, mabaki ya kale ya utamaduni ya Afrika yanayochukua 90% hivi bado yako katika nchi za Ulaya, kati yao mabaki elfu 70 hivi yanahifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Quai Branly.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Reuters, kwa muda mrefu sasa nchi za Afrika zimekuwa zikidai kurudishwa kwa mabaki ya kale ya utamaduni yaliyonyang’anywa wakati wa kipindi cha ukoloni. Aidha, taasisi na mashirika mengi ya Ulaya yamekuwa yakisaidia juhudi hizi za urejeshaji wa mali ya urithi wa utamaduni kwa Afrika. Matukio haya mawili ya Chuo cha Cambridge na Makumbusho ya Quai Branly kurudisha mali hiyo muhimu kwa nchi za Afrika yamefungua ukurasa mpya wa historia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma