

Lugha Nyingine
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kuongeza uelewano na urafiki: Mabalozi
NEW YORK – Konsela mkuu wa ubalozi wa China katika Mji wa New York nchini Marekani Huang Ping amesema kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 siyo tu itaongeza maelewano na urafiki kati ya nchi na sehemu mbalimbali, lakini pia itaongeza imani na matumaini kwa binadamu kushirikiana katika kukabiliana na changamoto.
Katika Makala yake iliyochapishwa wiki hii na Gazeti la Philadelphia Inquirer, Huang amewaalika wanamichezo kutoka Marekani na duniani kote kukusanyika pamoja mjini Beijing, kutimiza ndoto yao ya Olimpiki, kufahamu utamaduni wa China, na kusalia kumbukumbu zisizosahaulika za Olimpiki ya Majira ya Baridi maishani yao.
Huang ameongeza kuwa Michezo ya Olimpiki inatoa fursa nzuri kwa nchi na sehemu mbalimbali kukuza maelewano na urafiki, na kwamba mabadilishano kati ya watu kupitia michezo na utamaduni siku zote yamekuwa njia muhimu kwa uhusiano wa nchi mbili, akitolea mifano ya diplomasia ya mchezo wa mpira wa meza (Ping-Pong) na ziara ya Bendi ya Philadelphia nchini China miongo kadhaa iliyopita.
Amesema zaidi kwamba, China na Marekani zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya watu na utamaduni, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na uratibu wa mambo ya kimataifa kwenye msingi wa kuheshimu masuala ya makuu yanayofuatiliwa na kila upande na kushughulikia maoni ya tofauti kwa mwafaka, ili kuongeza mambo chanya mengi zaidi kwenye uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
“Katiba ya Olimpiki unaelekeza kwa uwazi kudumisha na kukuza uhuru na kutopendelea upande wowote wa kisiasa katika Michezo ya Olimpiki. Kuingiza siasa kwenye michezo kunaenda kinyume na mtazamo wa Katiba ya Olimpiki na kuharibu maslahi ya wanariadha kutoka nchi na sehemu mbalimbali" Ameandika Huang.
Kwa upande wake, Naibu Konsela wa Ubalozi ambaye pia ni Msemaji wa Ubalozi huo, Qian Jin amesema kwamba, ubalozi huo uko tayari kushirikiana na Marekani ili kuhimiza mawasiliano ya watu na ushirikiano wa kiviatendo kati ya China na majimbo yote ndani ya usimamizi wa ubalozi huo katika sekta za michezo, utamaduni, elimu na biashara.
Kwa mujibu wa Huang, Maandalizi yote kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 yako kwenye hatua za mwisho. “China itafanya kila juhudi kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi yenye mambo rahisi, salama na ya mazuri kwa dunia” ameandika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma