

Lugha Nyingine
China iko tayari kuionesha Dunia Michezo ya Olimpiki inayoandaliwa kirahisi, yenye usalama na ya murua
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2021
Hivi karibuni, serikali mbalimbali na kamati za michezo ya Olimpiki za nchi mbalimbali duniani zimeeleza matarajio na uungaji mkono kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022. Aidha, ofisi za ubalozi za nchi kadhaa zimefanya shughuli mbalimbali zinazohusu michezo hiyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema Jumatatu ya wiki hii hapa Beijing kuwa, “China iko tayari kuionesha Dunia Michezo ya Olimpiki inayoandaliwa kirahisi, yenye usalama na ya murua. Tuwapongeze pamoja wanamichezo hodari kutoka nchi mbalimbali na tuelekee siku za baadaye pamoja.”
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma