

Lugha Nyingine
“Ahadi ya Mashariki”: Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yashuhudia China kufungua mlango zaidi
Katika kando ya Mto Huangpu, mjini Shanghai, Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yamefunguliwa Alhamisi ya wiki hii.
Huku Mwaka 2021 ni mwanzo wa utekelezaji wa “Mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano” wa China, na pia ni maadhimisho ya miaka 20 tangu China ijiunge na Shirika la Biashara Duniani (WTO), China imebadilika kutoka nchi ya “kuuza bidhaa duniani kote” kuwa nchi ya “kununua kutoka duniani kote”.
Ikiwa nchi ya kufungua mlango zaidi, China imenufaika kwa fursa hii na pia kuleta manufaa kwa dunia.
Kufanyika kwa ubora zaidi
Eneo la maonesho ya nne ya CIIE limepanuliwa zaidi. Kuna nchi 15 zinazoshiriki kwenye maonesho hayo kwa mara ya kwanza. Kampuni 500 yenye nguvu zaidi za sekta mbalimbali duniani zinazoshiriki kwa mara nyingine kwenye maonesho hayo zimefikia asilimia 80. Maonesho hayo ya CIIE, yamekuwa yakifanyika kwa ubora zaidi kwa miaka mfululizo, yamekuwa jukwaa la Dunia la urahisi wa biashara za kimataifa, na ukanda mpya unaounganisha China na Dunia.
Ufanisi na Ushawishi Waongezeka
"Maonesho ya CIIE kwa Kampuni ya Danone ni jukwaa muhimu la kuonesha bidhaa mpya zenye uvumbuzi. Kutokana na ufanisi na ushawishi wa CIIE, tumeshaingiza bidhaa zaidi ya 30 kwenye soko la China" amesema Bw. Xie Weibo, Mkuu wa Kampuni ya Danone eneo la China na Oceania.
Vitu vilivyooneshwa vimebadilika kuwa bidhaa, huku washiriki wakibadilika kuwa wawekezaji. Baada ya kuendelezwa kwa miaka minne, maonesho ya CIIE yameunganisha China na Dunia, yakiwa ni maonesho ambayo yanaifanya dunia nzima inayoweza kunufaika pamoja. Wakati huo huo, idadi ya washiriki wake imeongezeka zaidi , matunda ya biashara na uwekezaji yamekuwa makubwa, na ufanisi na ushawishi wake unaendelea kuongezeka.
Dirisha la China, fursa ya Dunia
Kwa sasa, Dunia imefikia kipindi cha maendeleo makubwa, mabadiliko makubwa, na maboresho makubwa. Maambukizi ya virusi vya korona yameufanya uchumi wa Dunia uwe “njiapanda”.
Katika hali hiyo, China inayoendelea kupanua na kufungua mlango zaidi inavutia sana Dunia.
Tangu kuanza kwa maonesho ya CIIE yameunganisha soko la ndani na la kimataifa, na kuchangia rasilimali, siyo tu yametia nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi wa China yenye kiwango cha hali ya juu, bali pia yametoa fursa kwa ufufukaji na ukuaji wa uchumi wa Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma