

Lugha Nyingine
Sarafu ya kidijitali ya China yuan yaoneshwa kwa mara ya kwanza katika maonesho ya CIIE
SHANGHAI – Kwa mara ya kwanza China imeonesha sarafu ya kidijitali ya yuan au e-CNY ambayo inatumika kwenye mikahawa, vibanda, na mashine za kuuza katika Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE) yanayoendelea katika Jiji la Shanghai.
Maonesho ya nne ya CIIE, yamevutia takriban makampuni 3,000 kutoka nchi na sehemu 127. Wawakilishi wa biashara na washiriki wengine wa maonesho haya wanaweza kutumia sarafu ya China ya yuan iliyo katika mfumo wa kidijitali wanapolipia chakula au kununua zawadi za kumbukumbu kwenye maonesho.
Chu Yifeng, Mtendaji katika Benki kuu ya China (PBOC) amesema kwamba, Benki hiyo imeweka vibanda sita katika eneo la maonesho ya CIIE ili kusaidia wale wanaohitaji kuomba pochi ya kidijitali ya Yuan, na takribani karibu watu 60 hadi 80 wameripotiwa kwenda kwenye kila kibanda kutafuta msaada kila siku.
Katika duka la vikumbusho la Kituo cha Maonesho na Mikutano cha Shanghai, ambapo maonesho ya CIIE yanafanyika, watumiaji wanaweza kupata punguzo la asilimia 30 kwa kila Yuan za kidijitali 50 zitakazotumika katika kulipia huduma na bidhaa mbalimbali.
Punguzo pia hutolewa katika mikahawa ikiwemo ya Pizza Hut na KFC.
E-CNY ni toleo la dijitali la sarafu ya kiserikali iliyotolewa na Benki kuu ya China (PBOC) na kuendeshwa na watoa huduma walioidhinishwa. Ni chombo cha malipo kulingana na thamani, kulingana na akaunti sawa na msingi wa akaunti, chenye hadhi ya kisheria ya zabuni na muunganisho wa akaunti uliounganishwa bila udhibiti.
Uundaji wa mfumo wa e-CNY unalenga kuunda aina mpya ya RMB ambayo inakidhi mahitaji ya umma ya pesa taslimu katika zama ya uchumi wa kidijitali.
PBOC ilianza mradi wake wa utafiti na maendeleo wa e-CNY mwishoni mwa Mwaka 2017.
Hadi kufikia Juni 30, Mwaka 2021, e-CNY imetumika kwenye miamala zaidi ya milioni 1.32, inayohusu malipo ya huduma za umma, migahawa, usafiri, ununuzi na huduma za serikali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma