Katuni: Kuanzisha “Mpango wa Robin” na kudhibiti maoni ya umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2021

Katika wakati wa Vita Baridi, CIA ilianzisha “Mpango wa Robin” kwa kusudi la kuwaajiri waandishi wa habari na mashirika duniani kote ili kukusanya upelelezi na kuathiri maoni ya jamii kwa kupitia kudhibiti vyombo vya habari.

Mwandishi wa habari maarufu wa Marekani Carl Bernstein, ambaye alifichua undani wa hali ya mambo mwaka 1977, alisema kuwa kutokana na mpango huo, CIA iliwaajiri waandishi wa habari wengi kufanya ujasusi, na kuwataka waandishi hao kutunga “habari bandia”. CIA iliwahi kukiri kuwa, “Mpango wa Robin” ulikuwa umewaajiri waandishi wa habari zaidi ya 400 na mashirika makubwa 25 duniani kote.

Mpaka leo, CIA bado inachukua mbinu hii ovu ili kufikia kusudi lake la kufuatilia na kudhibiti maoni ya umma. Kwa serikali ya Marekani, ukweli wa habari hauna maana hata kidogo, na vyombo vya habari si chochote kingine ila ni chombo chake cha kudumisha umwamba wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha