

Lugha Nyingine
Bei ya mafuta yapanda kufuatia kuteremka kwa wiki
NEW YORK, Marekani - Bei ya mafuta duniani imepanda kwa kiasi kidogo Jumatatu ya wiki hii na kurejesha sehemu ya hasara walizopata wafanyabiashara wa sekta hiyo katika wiki iliyopita.
Kampuni ya West Texas Intermediate imeongeza senti za kimarekani 66 kwa utoaji wake mafuta katika Desemba, au asilimia 0.8, na kupata dola za kimarekani 81.93 kwa pipa kwenye Soko la Biashara ya bidhaa la New York. Mafuta ghafi ya Brent kwa ajili ya utoaji wa Januari yameongezeka senti za kimarekani 69, au asilimia 0.8, hadi kufikia dola za kimarekani 83.43 kwa pipa kwenye soko la ICE la London.
Wafanyabiashara wameendelea kutafakari uamuzi wa wazalishaji wakuu wa mafuta juu ya uzalishaji.
Shirika la Nchi Zinazouza Petroli na washirika wake, kwa pamoja lijulikanalo kama OPEC+, wiki iliyopita lilithibitisha kuwa litaendelea na mpango wake wa sasa na kuongeza uzalishaji kwa mapipa mengine 400,000 kwa siku (b/d) mwezi Desemba. Shirika hilo, linapunguza hatua kwa hatua upunguzaji wa uzalishaji uliofanywa mwaka jana.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa S&P Global Platts uliotolewa Jumatatu wiki hii, OPEC+ iliongeza uzalishaji wa mafuta ghafi kwa 480,000 b/d mwezi Oktoba, lakini ni nusu tu ya wanachama wa shirika hilo waliongeza uzalishaji mwezi uliopita.
Utafiti unasema wanachama wengi wa OPEC+ "wanajitahidi kuzalisha mafuta zaidi kama walivyoahidi".
Kwa mujibu wa kandarasi za mafuta za mwezi ujao, kwa wiki inayoishia Novemba 5, kiwango cha bei ya mafuta ghafi cha Marekani kilishuka karibu asilimia 2.8, huku Brent ikishuka kwa asilimia 1.2.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma