Lugha Nyingine
Rais wa China ahutubia mkutano wa APEC
(CRI Online) Novemba 12, 2021
Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa Shirika la Ushirikiano wa Uchumi la Asia na Pasifiki.
Katika hotuba yake, rais Xi amesema, janga la COVID-19 bado linaenea duniani, na nchi za Asia na Pasifiki zinapaswa kubeba majukumu ya kizama, kufanya kazi ya uongozi, na kusonga mbele kithabiti kwa lengo la kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja.
Pia rais Xi ametoa mapendekezo manne kuhusu kupambana na janga la COVID-19 kwa nguvu zote, kushikilia kufungua mlango na kufanya ushirikiano, kuhimiza kubadilisha njia ya kujipatia maendeleo ili kupunguza uchafuzi kwa mazingira, na kuhamasisha uvumbuzi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma