Katuni:Marekani yashtaki kwa mabavu meli ya“Yinhe” kwa kuchokoza China kwa makusudi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2021
Katuni:Marekani yashtaki kwa mabavu meli ya“Yinhe” kwa kuchokoza China kwa makusudi

Mwaka 1993, Marekani ilifanya uzushi kwa meli ya mzigo “Yinhe” ya China kwa umwamba wake.

Wakati huo, Marekani ikichukua kisingizio cha kupata upelelezi , ilijidai kuwa imepata “ushahidi wa kutosha” kuthibitisha meli ya mzigo“Yinhe” ilikuwa inapeleka raslimali ya silaha za kikemikali kwa Iran na kutishia kuiwekea China vikwazo. Wakati huo, Marekani ilipeleka manowari na helikopta kwenye bahari za kimataifa mahali ilipo Meli ya Yinhe.

Kwa kukabiliwa na shitaka hilo la Marekani lisilo na msingi wowote, China ililikanusha katakata. Baada ya uchunguzi, upande wa China uliiambia wazi Marekani kuwa havikuweko vitu vya kikemikali vilivyopigwa marufuku kwenye Meli ya Yinhe. Lakini Marekani bado ilijidai kuwa upelelezi ilioupata ni sahihi kabisa, na kushikilia kufanya ukaguzi kwa Meli ya Yinhe. Baadaye uchunguzi uliofanywa pamoja na upande wa tatu ulisema kuwa hakugunduliwa kwa raslimali yoyote ya kikemikali kwenye Meli ya Yinhe. Baada ya kutopata matokeo kwa ilivyotaka, Marekani ilifika hadi kujidai kuwa kitendo hicho kilifanyika “kwenye msingi wa kuamini upelelezi tofauti, ingawa upelelezi wote ni usio wa kweli .”

Jumuiya ya kimataifa ilikuwa imelaumu kitendo hicho, Gazeti la Jamhuri ya Kiislamu la Iran lilisema, serikali ya Marekani kuzusha tukio la Meli ya Yinhe, kitendo chake hicho ni cha “uharamia”. Gazeti la The Hindu lilisema, nchi ya Marekani iliyojidai ni “jaji mkuu wa dunia” ilizusha mgorogoro kwa makusudi lakini yenyewe ilipakwa matope.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha