Katuni: Marekani kuanzisha “Ofisi ya Mikakati” na kupamba “vita dhidi ya ugaidi”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2021

Baada ya tukio la “911” la mwaka 2001, wizara ya ulinzi wa nchi ya Marekani ilianzisha “Ofisi ya Mikakati”, ambayo ilibeba jukumu la kueneza propaganda kwa nchi za nje, kueneza habari za uwongo, na kupamba “vita vya Marekani dhidi ya Ugaidi”.

“Ofisi ya Mikakati” ilikuwa inatoa habari kwa vyombo vya habari vya nchi mbalibmali kwa kupitia mashirika yasiyo na uhusiano wazi na wizara ya ulinzi wa nchi ya Marekani, na kuwatumia viongozi na waandishi wa habari wa nchi mbalimbali baruapepe za kueneza maoni ya Marekani na kupinga serikali za nchi zenye uhasama na Marekani. Siku chache baada ya hapo, vilikuwepo vyombo vya habari vya Marekani vilivyosema kuwa, wizara ya ulinzi wa nchi ya Marekani ilitoa habari nyingi za uwongo kwa nchi mbalimbali, zikiwemo nchi zenye uhasama na Marekani pamoja na nchi za muungano wake.

Chini ya shinikizo kubwa la maoni ya watu, waziri wa ulinzi wa nchi wa Marekani wa wakati huo Donald Rumsfeld, alitangaza kufungwa kwa ofisi hiyo mnamo Februari, 2002. Wakati huo huo, alisema pia upande wa jeshi la Marekani hautaacha kazi za uenezi katika wakati wa vita. Mnamo Desemba, 2004, gazeti la “New York Times” lilitoa habari zikisema, Wizara ya Ulinzi wa nchi ya Marekani bado inajadili kama ingeweza au la na namna ya kudhibiti habari ili kushawishi watu wa nchi nyingine kukubali maoni ya Marekani.

Serikali ya Marekani ilifanya chini juu kudhibiti habari zilizotolewa kwa umma, ili kulitumikia lengo lake la kivita, ilificha kwa nguvu kubwa kusudi lake kweli la kuanzisha vita, na kwa kupitia propaganda za uwongo kujenga sura yake ya ati “kwa ajili ya haki na amani”. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha