Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Sita la Watu wa China na Afrika
Komgamano la Sita la Watu wa China na Afrika lilifanyika Beijing Jumatatu ya wiki hii Novemba 15.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alitumia barua ya pongezi kwa kongamano hilo.
Rais Xi Jinping alisisitiza kuwa Dunia ya hivi leo si tu ni ya zama za maendeleo makubwa bali pia ni ya zama za mabadiliko makubwa. Kwa kukabiliwa na fursa mpya na changamoto mpya, China na Afrika zinatakiwa kushikilia na kuenzi thamani ya pamoja ya amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru kwa binadamu wote kuliko wakati wowote uliopita, na kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuhimiza ustawi na maendeleo, na kujenga pamoja jumuiya ya binadamu ya mustakabali wa pamoja.
Natumai pande mbili za China na Afrika zitafanya jitihada za pamoja kulifanya Kongamano la Watu wa China na Afrika kuwa kiungo cha kuimarisha ushirikiano wa kina wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika, kuwa daraja la kuongeza maelewano kati ya watu wa China na Afrika, kuwa mfano mzuri wa kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, na kuanzisha hali mpya ya urafiki na ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma