Katuni: “kumbukumbu za Mtaa wa Downing” zafichua uwongo wa Marekani wa kuzusha vita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2021
Katuni: “kumbukumbu za Mtaa wa Downing” zafichua uwongo wa Marekani wa kuzusha vita

Mei 1, 2005, Gazeti la The Sunday Times la Uingereza lilitoa waraka mmoja wa kisiri kuhusu mkutano wa ndani wa serikali ya Uingeraza —— “kumbukumbu za Mtaa wa Downing” ambao ulifichua ukweli wa mlipuko wa vita vya Iraq.

Kumbukumbu hizo zilirekodi “matokeo” aliyojulisha Richard Dillov, aliyekuwa mkuu wa MI6 wa Uingereza baada ya kufanya ziara katika Marekani mwaka 2002. Dillov alisema, wakati huo serikali ya George W. Bush ilikuwa imeamua kuchukua vitendo vya kijeshi kwa kuangusha utawala wa Saddam wa Iraq, kwa sababu utawala wa Saddam ulishukiwa kuunga mkono ugaidi na kuwa na silaha za mauaji ya halaiki, lakini upande wa Marekani ulikuwa haujajadili matokeo yaliyowezekana kusababishwa na vitendo vyake vya kijeshi.

Mwaka 2013, Gazeti la “New York Times” lilichapisha makala ikisema, kuzusha vita vya Iraq kulitokana na kupotosha hali halisi kwa makusudi, na waraka wa ”kumbukumbu za Mtaa wa Downing” ni ushahidi mzuri kabisa. Utawala wa Saddam ulikuwa hauna silaha za mauaji ya halaiki , pia haukuhusika na “tukio la 9.11”.

Ukweli wa mambo yasiyohesabika, na hali ya kumwaga damu vimeonesha kuwa, Marekani ilijua wazi hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha Utawala wa Saddam kuwa na silaha za mauaji ya halaiki, lakini ilizusha kisingizo kwa ilivyopenda ili kuanzisha vita, ambapo umwamba wake uliotegemea uwongo umeonekana wazi kabisa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha