Lugha Nyingine
Biashara ya nje ya Kenya yaongezeka huku vizuizi dhidi ya UVIKO-19 vikilegezwa
NAIROBI – Biashara ya nje ya Kenya imeripotiwa kuongezeka kwa wastani wa asilimia 15.6 katika kipindi cha kati ya Mwezi Januari hadi Agosti na kufikia shilingi bilioni 490 za Kenya sawa na dola bilioni 4.37 za Marekani, ikilinganishwa na dola bilioni 3.78 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho Mwaka 2020.
Taarifa iliyotolewa Jumanne hii na Wakala wa Kukuza Biashara ya Nje na Chapa ya Kenya (KEPROBA) imehusisha kupanda kwa mapato ya biashara ya nje na juhudi za nchi hiyo za kupunguza utegemezi wake kwa soko la kilimo lisilo na utulivu.
"Kulegezwa kwa hatua za kuzuia maambukizi ya UVIKO-19 katika soko letu la nje pia imetusaidia" Wilfred Marube, Mkurugenzi Mtendaji wa wakala huyo wa Serikali amesema.
Marube amesema Kenya imejaribu kuuza bidhaa za aina mbalimbali katika nchi za nje.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na KEPROBA, bidhaa kuu zinazouzwa nje ni pamoja na mazao yanayotokana na kilimo cha bustani, chai, mavazi na nguo, kahawa, madini, bidhaa za mafuta ya petroli, mafuta yatokanayo na wanyama na mimea, mashine na vipuri vya mashine, bidhaa za chuma pamoja na dawa za binadamu.
Baadhi ya masoko yanayoagiza bidhaa kutoka Kenya kwa wingi ni pamoja na nchi za Uganda, Uingereza, Pakistani, Tanzania na Misri.
“Kenya inazingatia fursa zinazotolewa katika Maonesho ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya Mwaka 2020 yanayoendelea huko Dubai, Falme za Kiarabu” Marube amenukuliwa akisema.
Amebainisha kuwa Kenya inashiriki katika maonesho hayo na inaonesha ubora wake katika utalii, biashara, uwekezaji, utamaduni, michezo, miongoni mwa mambo mengine muhimu.
Marube ameongeza kuwa, maonesho hayo ni lango la Kenya la kukuza mauzo ya nje siyo tu kwa eneo la Ghuba lakini kwa dunia nzima.NAIROBI – Biashara ya nje ya Kenya imeripotiwa kuongezeka kwa wastani wa asilimia 15.6 katika kipindi cha kati ya Mwezi Januari hadi Agosti na kufikia shilingi bilioni 490 za Kenya sawa na dola bilioni 4.37 za Marekani, ikilinganishwa na dola bilioni 3.78 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho Mwaka 2020.
Taarifa iliyotolewa Jumanne hii na Wakala wa Kukuza Biashara ya Nje na Chapa ya Kenya (KEPROBA) imehusisha kupanda kwa mapato ya biashara ya nje na juhudi za nchi hiyo za kupunguza utegemezi wake kwa soko la kilimo lisilo na utulivu.
"Kulegezwa kwa hatua za kuzuia maambukizi ya UVIKO-19 katika soko letu la nje pia imetusaidia" Wilfred Marube, Mkurugenzi Mtendaji wa wakala huyo wa Serikali amesema.
Marube amesema Kenya imejaribu kuuza bidhaa za aina mbalimbali katika nchi za nje.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na KEPROBA, bidhaa kuu zinazouzwa nje ni pamoja na mazao yanayotokana na kilimo cha bustani, chai, mavazi na nguo, kahawa, madini, bidhaa za mafuta ya petroli, mafuta yatokanayo na wanyama na mimea, mashine na vipuri vya mashine, bidhaa za chuma pamoja na dawa za binadamu.
Baadhi ya masoko yanayoagiza bidhaa kutoka Kenya kwa wingi ni pamoja na nchi za Uganda, Uingereza, Pakistani, Tanzania na Misri.
“Kenya inazingatia fursa zinazotolewa katika Maonesho ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya Mwaka 2020 yanayoendelea huko Dubai, Falme za Kiarabu” Marube amenukuliwa akisema.
Amebainisha kuwa Kenya inashiriki katika maonesho hayo na inaonesha ubora wake katika utalii, biashara, uwekezaji, utamaduni, michezo, miongoni mwa mambo mengine muhimu.
Marube ameongeza kuwa, maonesho hayo ni lango la Kenya la kukuza mauzo ya nje siyo tu kwa eneo la Ghuba lakini kwa dunia nzima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma