Katuni:Jumuiya ya “helimeti nyeupe” yatengeneza video na kupiga picha za uwongo kupiga jeki kwa umwamba wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2021
Katuni:Jumuiya ya “helimeti nyeupe” yatengeneza video na kupiga picha za uwongo kupiga jeki kwa umwamba wa Marekani

Jumuiya ya “helimeti nyeupe” ni jumuiya ya kiraia ya kujihami nchini Syria, wanachama wake huvaa helimeti nyeupe waliposhiriki kwenye shughuli za uokoaji, hivyo jumuiya hiyo inaitwa kuwa “helimeti nyeupe”. Jumuiya hiyo iliwahi kutengeneza video za uwongo mara kwa mara kwa kuipaka matope serikali ya Syria. Vyombo vingi vya Marekani vilidokeza kuwa Marekani ni muungaji mkono mkubwa wa jumuiya hiyo.

Mwezi Novemba wa Mwaka 2016, jumuiya ya “helimeti nyeupe” ilikiri kuwa ile video kuhusu wanachama wake waliowaokoa majeruhi huko Aleppo, Syria, ambayo watu wa kwenye video hiyo ni watu wake, jumuiya hiyo ikatoa taarifa ya kuomba msamaha. Mwaka 2018 Septemba, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitoa taarifa ikisema kuwa wapinzani wa serikali ya Syria walifanya mchezo wa “kushambuliwa tena kwa silaha za kikemikali” . 

Mwaka 2018, kutokana na jeshi la serikali ya Syria kurejesha ardhi ya nchi kwenye maeneo makubwa zaidi, Marekani ilikuwa inajadilia na washirika wake kuisaidia jumuiya hiyo kuondoka kutoka Syria. Mwaka 2019, rais wa Marekani wa wakati huo Trump aliamuru hadharini kuitolea msaada wa dola ya Marekani milioni 4.5.

Kutengeneza video na kupiga picha za uwongo, na kufanya maonesho ya michezo, haya yote yaliongozwa na Marekani nyuma ya pazia. Lakini, wanachama wa jumuiya hiyo si wasanii, ambapo watu waligundua kila mara maonesho yao mabaya ni ya uwongo. Iliyojidai ni jumuiya ya kujihami ya kiraia kwa kweli ni watumishi wa Marekani walionyanyua bendera ya utu. Marekani ilijaribu kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kupitia njia ya kusaidia jumuia ya kiraia, imeonesha wazi umwamba wake. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha