Katuni: Marekani yaanzisha mpango wa “kusafisha mtandao” na kudumisha nafasi yake ya umwamba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2021

Tarehe 5, Agosti, mwaka 2020, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati huo Mike Pompeo alianzisha mpango wa “kusafisha mtandao” uliolenga kampuni za China, ambao ukitumia kisingizio kwamba kampuni za China zimekuwa “tishio kubwa” dhidi ya usalama wa nchi ya Marekani na faragha za raia, ulijaribu kuibana kampuni ya Huawei na kampuni nyingine za China katika sekta ya 5G. Ili kutembeza mpango huo, Pompeo na Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati huo Keith J. Krach walikwenda nchi mbalimbali kuwashawishi watu .

Lakini “Gazeti la Kioo” la Ujerumani zilitoa habari zikisema, baada ya kufanya uchunguzi kwa miaka mingi, Umoja wa Ulaya, na mashirika ya kiserikali ya Uingereza na Ujerumani zilikuwa hazijagundua matatizo ya usalama ya vifaa vya HUAWEI, badala yake zinaweza kugundua mara kwa mara matatizo ya usalama kwenye vifaa vya kampuni ya Cisco ya Marekani.

Marekani inazusha uwongo na kuzipaka matope kampuni za China kwa kusudi lake kweli la kudumisha hali yake ya kuhodhi sekta ya teknolojia na kudumisha umwamba wake. Ukweli wa mambo ni kuwa, Marekani ndiyo nchi yenye tishio dhidi ya usalama wa mtandao wa intaneti wa dunia nzima. Mwandishi wa vitabu wa Uingereza Tom Fowdy, ambaye pia ni mtaalam wa masuala ya kimataifa alisema, kampuni kubwa kama vile Google, Microsoft, Amazon, Facebook n.k. zote ni kampuni za Marekani. Kampuni hizo zinatoa data za tarakimu kwa serikali ya Marekani, ili iweze kujenga mtandao wa kufuatilia na kudhibiti dunia nzima.

Marekani inafanya chini juu kwa kubana kampuni za teknolojia za China bila ya sababu yoyote, kutumia nguvu ya nchi kwa inavyopenda, na kuharibu kanuni ya soko, matokeo yake hakika ni kuleta vurugu kwenye soko la kimataifa, kuwadhuru wengine na kujidhuru.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha