Putin akubali kwa furaha mwaliko wa kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2021

Kwa mujibu wa ripoti, Msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov hivi karibuni alisema kuwa Rais Vladimir Putin amepokea mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China wa kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 , na baada ya Russia na China kukubaliana katika masuala yote, pande hizo mbili zitatangaza kwa pamoja habari husika.

Siku ya Jumatatu ya wiki hii, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alipojibu maswali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa kushiriki matukio makubwa kwa pamoja ni desturi nzuri ya miaka mingi kati ya China na Russia.

Zhao amesema kuwa, Mwaka 2014, Rais Xi Jinping alialikwa kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Sochi, kwa mara hii, Rais Xi Jinping amemwalika rafiki yake mzuri Rais Putin kuja China kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Rais Putin kwa furaha amekubali mwaliko huo. Pande hizi mbili zimekuwa zikiendelea kuwasiliana kuhusu masuala husika ya ziara ya Rais Putin hapa China.

“Naamini miadi ya marais hawa wawili ya kukutana kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi yatathibitisha tena uhusiano wa kirafiki na ujirani mwema wa China na Russia. Ninaamini kuwa wanamichezo wa nchi hizi mbili watapata mafanikio mapya na kutoa mchango kwa ajili ya kuionesha Dunia Michezo inayoandaliwa kirahisi, yenye usalama na ya murua.” (Mwandishi wa habari: Wu Yue, Zhu Chao) 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha