Afrika Kusini na Kenya zakubaliana kuinua uhusiano kuwa wa kimkakati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2021

JOHANNESBURG - Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ni wakati wa kuinua uhusiano kati ya nchi hiyo na Kenya kuwa "ushirikiano wa kimkakati."

Rais Ramaphosa amesema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika majengo ya Muungano mjini Pretoria siku ya Jumanne ya wiki hii.

Viongozi hao wawili wamesisitiza umuhimu wa uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza dhamira yao ya kuinua uhusiano huo kupitia kufikia Mkataba wa Ushirikiano wa Kimkakati.

Wakati nchi hizo mbili zikipanga kuimarisha biashara na uwekezaji, Ramaphosa amedokeza kuwa kuinua uhusiano kunaweza kuwa muhimu kwa sekta nyingine.

Kenyatta yuko ziarani nchini Afrika Kusini hadi Jumatano ya leo.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kutathmini hali ya sasa ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili huku pia ikitoa fursa ya kutazama maeneo mapya yenye maslahi na manufaa kwa watu wa Afrika Kusini na Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha