Tanzania na China ni marafiki wa siku zote : Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Liberata Mulamula katika Mahojiano maalum

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2021
Tanzania na China ni marafiki wa siku zote : Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Liberata Mulamula katika Mahojiano maalum
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Liberata Mulamula akiwa katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua huko Dar es Salaam Novemba 18, 2021. (Mpiga picha: Herman Immanuel)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Liberata Mulamula alisema “Tanzania na China ni marafiki wakubwa wa siku zote , uhusiano kati ya nchi zetu mbili umekuwa mzuri zaidi na wa kina zaidi.”

Waziri Mulamula alisema hayo katika mahojiano ya hivi karibuni na mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua yaliyofanyika hivi karibuni Dar es Salaam, Tanzania.

 Kuhusu Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika Dakar, Mji Mkuu wa Senegal mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba kuanzia Tarehe 29-30. Bibi Mulamula amesema, Tanzania imekuwa ikihudhuria kwenye mikutano yote ya mawaziri na ya kilele iliyofanyika.

Amebainisha kuwa, yeye pia amekuwa akihudhuria kwenye mikutano ya Baraza hilo la Ushirikiano wa China na Afrika na kwamba ameshuhudia namna uhusiano kati ya Afrika na China ulivyopandishwa ngazi mara mbili kutoka uhusiano wa wenzi wa aina mpya kuwa uhusiano wenzi wa kimkakati wa aina mpya na baadaye kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa ushirikiano wa pande zote.

“Mwanzoni ushirikiano kati ya Tanzania na China ulijikita kwenye sekta chache tu, lakini sasa umepanuka katika sekta nyingi” alisema.

Bibi Mulamula alisema, baada ya kupata uhuru, Tanzania ilijikita katika juhudi za kuendeleza uchumi wa kitaifa na kuunga mkono harakati za ukombozi wa nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika. 

Amebainisha kuwa, Reli ya TAZARA iliyojengwa kwa msaada wa China imekuwa ikiwezesha nchi ya Zambia ipate njia mpya ya kuunganishwa na bandari kwenye Bahari ya Hindi.

“Sasa, urafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na China unaonekana katika nyanja nyingi zaidi, kama vile:uwekezaji,ujenzi wa miundombinu, ukuzaji wa viwanda na kadhalika”.Amesisitiza kwamba, baada ya kuundwa kwa serikali ya awamu mpya ya Tanzania, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiimarishwa zaidi. Amesema, Tanzania iko tayari kutumia fursa mpya nyingi zaidi za ushirikiano wa kimkakati, ili kutimiza maendeleo ya kunufaishana .

Bibi Mulamula alisifu “ Pendekezo la China kuhusu Maendeleo ya Dunia nzima”. Amesema , kuenea kwa maambukizi ya virusi vya korona kumedhihirisha kuwa nchi zote duniani ni za jumuiya moja, hakuna nchi yoyote inayoweza “kuachwa nyuma”. 

Akizungumzia ushirikiano wa siku za baadaye kati ya Afrika na China Mulamula alisema, Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika(AfCFTA) lililoanzishwa mwaka huu limetoa muktadha mpana kwa ushirikiano wa Afrika na China katika siku za baadaye na sekta ya viwanda ya Afrika inatarajiwa kupata maendeleo. 

Miaka 21 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, uhusiano kati ya pande hizo mbili kwenye msingi wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana umeendelea kuwa karibu zaidi na maendeleo makubwa zaidi yatafikiwa katika siku za baadaye.

Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua: Xie Hao 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha