Benki Kuu ya Tanzania yakadiria ongezeko la uchumi kufikia asilimia 5 Mwaka 2021

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2021

DAR ES SALAAM - Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Florens Luoga, amesema Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5 Mwaka 2021.

"Kwa kutupia macho miaka ya baadaye, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kuongezeka kwa madhubuti, na kufikia zaidi ya asilimia 8 katika kipindi cha miaka mitano ijayo," Luoga amesema Alhamisi ya wiki hii katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha unaofanyika Dodoma, Mji Mkuu wa Tanzania.

Luoga amesema makadirio hayo yanategemea ongezeko la ufanisi wa matumizi rasilimali na tija.

Amesema ingawa Tanzaniahai haikuchukua hatua kali za udhibiti wa janga la UVIKO-19 hasa kutofunga shughuli za kiuchumi, nchi hiyo haijaepushwa na athari mbaya za kiuchumi zinazosababishwa na janga hilo.

Luoga amebainisha kwamba, ongezeko la uchumi lilipungua hadi kufikia asilimia 4.8 Mwaka 2020, kutoka wastani wa asilimia 6.8 kwa miaka mitano iliyopita.

Ameongeza kuwa utalii, ambao ni chanzo kikuu cha fedha za kigeni, uliathiriwa vibaya na janga hilo kwani mapato yalipungua kwa zaidi ya nusu hadi dola za kimarekani milioni 714.5 Mwaka 2020, kufuatia kupungua kwa watalii kwa takriban asilimia 60.

Mkutano huo wa siku mbili umevutia zaidi ya wataalam 300 wa ndani na wa nchi za nje ili kufikiria upya jinsi ya kuwezesha ufufukaji wa haraka wa uchumi na kuhakikisha ukuaji endelevu baada ya UVIKO-19. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha