Uchunguzi wa Kimataifa: Marekani inayofuata demokrasia kwa kujionesha haina sifa ya kuwa Mwalimu wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2021

Alhamisi ya wiki hii, Marekani itaitisha kile kinachoitwa “Mkutano wa kilele wa Demokrasia wa Viongozi ”. Lakini maoni ya watu wengi ya jumuiya ya kimataifa ni kuwa, Marekani imepoteza hadhi yake ya kimaadili kufundisha uzoefu wa demokrasia kwa Dunia.

Kwa mujibu wa kura ya maoni ya watu iliyoendeshwa na Taasisi ya Pew Mwezi Juni mwaka huu, ni asilimia 14 tu ya raia wa Ujerumani wanaona demokrasia ya Marekani inastahiki kufuatwa. Uchunguzi uliofanywa katika nchi za Ufaransa, Uingereza, Korea Kusini, Japan, Australia na New Zeland pia umepata matokeo kama hayo. Gazeti la Washington Post lilidhihirisha kwa masikitiko kuwa, nchi washirika wa Marekani zinaona demokrasia ya Marekani imeanguka, na ni ya wakati uliopita na “kuisha kabisa”.

Wachambuzi kwa ujumla wanaamini kwamba, fujo iliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu kwenye Bunge la taifa la Marekani ni alama iliyofunua kificho cha “Hadithi ya Demokrasia ya Marekani”. Kwa sababu ya kutokubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Mwaka 2020, makundi ya “ watu wenye fujo” yalivamia Bunge la taifa la Marekani, ambalo ni jiwe la msingi la mamlaka ya umma.

Badala ya kusema fujo hizo za Bunge la taifa la Marekani zilikuwa ni sababu ya kuanguka kwa hadithi ya demokrasia ya Marekani, ni bora kusema kwamba ni dalili ya ugonjwa wa kimfumo wa demokrasia ya Marekani.

Demokrasia si mapambo, badala yake inahitaji kutatua matatizo ya binadamu. Katika Marekani ya hivi sasa, idadi ya watu waliofariki kutokana na korona imepita ile ya vita vyote Marekani ilivyoanzisha au imeshiriki. Makundi ya watu walio wachache yanakabiliwa na ubaguzi na dhuluma katika sekta za elimu, ajira na huduma za matibabu; Makumi na maelfu ya raia wanakufa kwa sababu ya mabavu ya kisilaha; Watoto wakimbizi walioko kwenye mipaka kati ya Marekani na Mexico wanakaa kama dagaa kwenye nafasi finyu na kuishi maisha magumu. Kura za maoni ya watu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Wamarekani wanalalamika hali ya demokrasia ya nchi hiyo.

Katika wakati wa uchaguzi, wapigakura wanavutiwa kwa kila njia, na wanasiasa hupuuza mahitaji yao kabisa baada ya uchaguzi kuisha, demokrasia kama hiyo bila shaka ni uongo tupu. Mnamo Mwaka 1988, Makamu wa Rais wa Marekani wa wakati huo George H. Bush alipogombea nafasi ya urais alitoa ahadi inayovutia sana: kutoongeza kodi mpya. Lakini miaka miwili baada ya kuingia madarakani, Bush alikiri kuwa, kuurejesha uchumi wa Marekani katika hali nzuri kunahitaji hatua mfululizo, ikiwemo “kuongeza kodi".

Ni demokrasia ya kusisimua wapigakura wakati wa uchaguzi na kuacha baadhi ya ahadi baada ya uchaguzi. Bush si Rais pekee wa Marekani aliyefanya hivyo. Takwimu zinaonesha kwamba ni asilimia 48 tu ya ahadi 535 zilizototolewa na Rais Barack Obama wakati wa uchaguzi zilitimizwa; na namba hiyo kwa Rais Donald Trump ni asilimia 21.

Rais wa sasa Joe Biden wa Marekani kwenye kampeni za uchaguzi aliahidi kuwa, anataka “mshikamano na uponyaji”, na kutarajia msimamo wa fufutende. Lakini vyombo vya habari vya Marekani vimedhihirisha kuwa, hali ya hivi sasa inaonekana kuwa Biden anachukua hatua kali. Jalida la Capitol Hill lilisema, kitendo cha Biden kuwa kigeugeu kimeongeza hali ya raia kutoamini serikali.

Mavazi ya kupendeza ya demokrasia ya Marekani yamejaa matundu, lakini nchi hiyo inazicheka nchi nyingine kwa kuvaa “nguo rahisi na safi”. Mfumo wa demokrasia wa unafiki, wa kushindwa kufanya kazi, wa kudhoofika, wa kudanganya na wa kujionesha hauna sifa ya kuwa mwalimu wa demokrasia wa Dunia nzima. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha