Lugha Nyingine
Xi asisitiza kufuata njia utekelezaji wa sheria za ujamaa wenye umaalum wa China
Sherehe ya kuadhimisha miaka 100 toka kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ikifanyika katika Uwanja wa Tian'anmen wa Beijing, Julai 1, 2021. (Xinhua/Chen Zhonghao) |
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza kufuata njia ya utekelezaji wa sheria ya ujamaa wenye umaalum wa China, na kuhimiza ujenzi wa mfumo wa utekelezaji wa sheria.
Xi amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye semina elekezi ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Jumatatu ya wiki hii.
Akibainisha kuwa China sasa iko katika hatua muhimu ya kufikia ustawishaji wa taifa, Xi amehimiza juhudi za kuinua uwezo na kiwango cha utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria katika mambo yote, na kutoa hakikisho thabiti la kisheria kwa ajili ya kujenga nchi ya kijamaa ya mambo ya kisasa kwa pande zote.
Mfumo wa utawala wa nchi kisheria wa kijamaa wenye umaalum wa China unapaswa kuendelezwa kwa kina, Xi ameongeza kwa kusema kuwa juhudi zinapaswa kufanywa ili kuzingatia mwelekeo sahihi katika kujenga mfumo wa utekelezaji wa sheria, kudumisha uongozi wa CPC na mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China, na kutekeleza nadharia ya utekelezaji wa sheria ya kijamaa ya China.
Xi ametoa wito kwa juhudi zaidi za kukuza kazi ya kutunga sheria katika maeneo muhimu yakiwemo Usalama wa Taifa, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, afya ya umma, usalama wa viumbe na ulinzi wa viumbe, uhifadhi wa mazingira na kuzuia hatari, na kuweka mkazo katika kuinua ubora wa sheria.
Akitoa wito wa kuboreshwa kwa utaratibu wa kuhakikisha kuwa kila mtu ana haki sawa mbele ya sheria, Xi amesema kuwa vitendo vyote vinavyokiuka Katiba ya Nchi au sheria nyingine lazima viwajibike.
Xi pia ametaka kuongezwa kwa usimamizi juu ya utungaji wa sheria, utekelezaji wa sheria, uendeshaji wa mashitaka, na mamlaka ya mahakama, na kuboresha mafunzo ya watendaji wa sheria.
Xi amehimiza jitihada zinazoendelea za kukabiliana na rushwa katika utekelezaji wa sheria na mahakama kwa mujibu wa sheria, kupambana na uhalifu wa kupangwa na kung'oa magenge ya wahalifu wa ndani kwa misingi inayoendelea.
Akisisitiza kuimarishwa kwa utekelezaji wa sheria katika maeneo yanayohusiana na mambo ya nje, Xi ametoa wito wa kuhimiza maendeleo ya mfumo wa utekelezaji wa sheria kwa ajili ya matumizi ya nje ya mipaka ya nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma