

Lugha Nyingine
Msemaji wa China: Marekani "italipa gharama" kwa hatua zake zisizo sahihi dhidhi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian ameeleza kuwa Marekani "italipa gharama” kwa ajili ya hatua zake zisizo sahihi".
Msemaji huyo amesema hayo Jumanne ya wiki hii wakati alipozungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na China kwa kujibu taarfia iliyotolewa na Ikulu ya Marekani kwamba nchi hiyo haitatuma ujumbe wowote wa kidiplomasia au rasmi kuhudhuria Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022.
"China imelalamikia na kupinga vikali kauli hiyo ya Marekani," Zhao amesema katika mkutano na waandishi wa habari. "China imetoa malalamiko kwa Marekani, na itachukua hatua za kulipiza dhidi yake."
Amesema kwamba, vitendo vya Marekani vinakiuka kwa kiasi kikubwa kanuni ya kutoegemea upande wowote kisiasa iliyothibitishwa kwenye Katiba ya Olimpiki, vinaenda kinyume na kauli mbiu ya Olimpiki ya "mshikamano", na vinasimama kinyume na wanamichezo wa kimataifa na mashabiki wa michezo kote duniani.
Zhao amebainisha kwamba, kwa mujibu wa kanuni za Olimpiki, maafisa wanaalikwa na Kamati ya Olimpiki ya nchi yake kuhudhuria Michezo ya Olimpiki, na kama maafisa wa Marekani watakuja au la kuhudhuria Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na kuwatia nguvu wanamichezo wao ni suala lenyewe la Marekani.
Ameongeza kuwa, licha ya kutokualikwa, Marekani inahusisha kuhudhuria kwa maafisa wake na kile kinachoitwa masuala ya haki za binadamu ya Xinjiang, hali ambayo ni kwenda njia potofu na kujidanganya wao wenyewe na wengine.
"Ajenda ya kisiasa ya Marekani haipati uungwaji mkono na hakika itashindwa," Zhao amesema.
Zhao ameitaka Marekani kuacha kuingiza siasa kwenye michezo na kuvuruga na kudhoofisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, isije ikaathiri mazungumzo na ushirikiano katika sekta muhimu na masuala ya kimataifa na kikanda kati ya pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma