Rais Xi Jinping wa China atuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini 2021

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2021

Jumatano ya wiki hii, Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini 2021 ambalo limeanza Beijing, Mji Mkuu wa China.

Katika barua hiyo, Xi amedhihirisha kuwa, haki za binadamu ni alama ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Kujali maisha ya watu, thamani na heshima ya binadamu, na kuwezesha kila mtu awe na haki za binadamu, huu ni utafutaji wa pamoja wa jamii ya binadamu. Kuzingatia ukuu wa watu, na kuchukulia matarajio ya umma juu ya maisha bora kuwa lengo la kufanya juhudi, huu ni wajibu wa zama kwa nchi zote duniani.

Xi amesisitiza kuwa, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku zote ni chama kinachoheshimu na kuhakikisha haki za binadamu. China inashikilia kuweka umma katikati, na kuweka mbele maslahi ya umma, kuhimiza haki za binadamu katika hali ya kujipatia maendeleo, kuendeleza demokrasia ya watu katika mchakato mzima, na kuhimiza maendeleo huru ya watu katika nyanja zote, na kwa mafanikio China imefuata njia ya kuendeleza haki za binadamu inayoendana na mawimbi ya zama, na kupata mafanikio dhahiri katika kuhimiza mambo ya haki za binadamu ya China, ambapo watu wa China wapatao zaidi ya bilioni 1.4 wamezidi kupata uhakikisho, furaha na usalama katika haki za binadamu. Uzoefu katika mambo ya haki za binadamu ni wa aina mballimbli. Watu wa nchi mbalimbali duniani pia wanatakiwa kuchagua kwa uhuru njia ya kuendeleza haki za binadamu inayolingana na hali halisi ya nchi zao. China ingependa kujiunga pamoja na nchi mbalimbali zinazoendelea katika kuenzi thamani ya pamoja ya binadamu wote, kufanya ushirikiano wa pande nyingi, ili kuchangia busara na nguvu za kuwezesha mambo ya haki za binadamu ya kimataifa yaendelee vizuri.

Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini 2021 umefunguliwa hapa Beijing siku hiyo, ukiwa na kaulimbiu ya “Umma Kwanza na Kushughulikia Haki za Binadamu za Dunia Nzima ”, umeandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China na Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha