China na Rwanda zasaini makubaliano ya kupunguza ulipaji kodi mara dufu

(CRI Online) Desemba 09, 2021

China na Rwanda zimesaini makubaliano ya kupunguza kodi mara dufu kwa kodi za Mapato na Kuzuia Ukwepaji Kodi pamoja na taratibu zinazohusiana nazo.

Makubaliano hayo yalisainiwa Kigali, Mji Mkuu wa Rwanda Jumanne ya wiki hii na Balozi wa China nchini Rwanda Rao Hongwei na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Uzziel Ndagijimana.

Baada ya tukio la kusaini makubaliano hayo, Balozi Rao alisema ushirikiano kwenye masuala ya kodi kati ya nchi mbili una umuhimu mkubwa katika kufanya uhusiano wa kibiashara wa pande mbili uendelee vizuri na kudumu.

Ameongeza kusema kwamba, kusainiwa kwa makubaliano hayo pamoja na taratibu zake nyingine kutapunguza sana mzigo wa kodi wa walipa kodi wanaowekeza katika pande zote mbili na kusukuma mbele ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili pamoja na mabadilishano ya wafanyakazi.

Kwa upande wake Ndagijimana amesema kwamba, makubaliano hayo yataboresha nafasi ya Rwanda kama sehemu nzuri ya uwekezaji kwa Kampuni za China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha