

Lugha Nyingine
Idara ya Kustawisha Vijiji ya China Kuanzisha Ushirikiano wa Kiwenzi kati ya China na Afrika Kupunguza Umaskini na kujipatia maendeleo
Mkuu wa Idara ya Kustawisha Vijiji ya China Liu Huanxin amesema hivi karibuni kwamba, wakati China inapoondoa umaskini, siku zote imekuwa mtetezi, msukuma mbele na mtoa mchango muhimu kwa ajili ya kutimiza lengo la kimataifa la kupunguza umaskini na kustawisha vijiji. “Tuna nia ya kuendelea kufanya mabadilishano ya kirafiki na ushirikiano na nchi za Afrika kuhusu kupunguza umaskini na kustawisha vijiji, kuanzisha ushirikiano wa kiwenzi wa kupunguza umaskini na kujipaptia maendeleo kati ya China na Afrika”
Liu Huanxin amesema hayo kwenye “Mkutano wa Kupunguza Umaskini na kujipatia Maendeleo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika la 2021” ambao uliandaliwa na Idara ya Kustawisha vijiji ya China. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya video, na ulikuwa na kaulimbiu isemayo “Ushirikiano kati ya China na Afrika: Sera na Uzoefu wa maendeleo vijijini”.
Liu Huanxin amesema, mafanikio makubwa ya China katika kuondoa umaskini yamehimiza mchakato wa kupunguza umaskini duniani kote, yameimarisha imani ya kupunguza umaskini kwa jumuiya ya kimataifa, na kutoa mchango wa busara na suluhisho za China katika kupunguza umaskini na kustawisha vijiji duniani.
“Baada ya kumaliza kazi ngumu ya kutokomeza umaskini wa kupindukia, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Serikali ya China zimezifanya kazi kuhusu “kilimo, vijiji na wakulima” ziweke mkazo katika kuendeleza kwa kina ustawishaji wa vijiji katika nyanja zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma