Mwenyekiti Kamati ya IOC asema kuongezeka kwa mivutano ni kinyume na dhamira ya IOC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2021
Mwenyekiti Kamati ya IOC asema kuongezeka kwa mivutano ni kinyume na dhamira ya IOC
Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 ukiwa kwenye Mnara wa Olimpiki wa Beijing. (Xinhua/Wang Yong)

BERLIN - Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach amesema kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 haipaswi kutumiwa kwa kuongeza hali ya mivutano duniani na kwamba ushiriki wa wanamichezo ni makubaliano ya kimataifa.

Bach ameelezea wasiwasi wake kuhusu ushiriki wa wanamichezo baada ya Marekani kutangaza kutotuma maafisa wa serikali kuhudhuria mashindano hayo yatakayofanyika Beijing mapema Mwaka 2022 kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao Jumatano ya wiki hii baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya IOC, Bash alikaribisha uungwaji mkono wote kwa timu za Olimpiki ili kuwapa wanamichezo uhakika.

"Hii ni kwa mujibu wa makubaliano yaliyopitishwa na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaounga mkono Azimio la Kusimamisha vita wakati wa Olimpiki," Bach amesema.

"Kuwepo kwa maafisa wa serikali ni uamuzi wa kisiasa. Kutofungamana na upande wowote kisiasa kunazingatiwa na IOC haitafungamana na upande wowote."

Kwa mujibu wa Bach, IOC inaandaa michezo hiyo kwa ajili ya kuunganisha Dunia nzima, siyo kuigawanya. Aliichukulia Michezo ya Olimpiki ya zama za kale kama mfano ili kuthibitisha kwamba kuingilia kisiasa kutaharibu na kumaliza Michezo hiyo.

"Tunaishi katika dunia hii yenye mapambano na ufarakanishaji ambapo hali ya wasiwasi inaongezeka. Kama Michezo ya Olimpiki itaongeza hali hiyo, itakuwa kinyume kabisa na kazi yetu," amesema Bach.

Bach anaamini kazi na wajibu wa IOC ni kuhakikisha kila kitu kinachohusiana na Michezo ya Olimpiki na Mkataba wa Olimpiki na hakuna shaka kwamba washirika wa China watatimiza ahadi kama walivyofanikiwa katika mashindano ya jaribio.

"Mkataba wa kuendesha mashindano unaheshimiwa kikamilifu. Unajumuisha kuheshimu haki za binadamu kwa washiriki wote na masuala mengine kadhaa. Na katika suala hili, tunafanya kazi kwa karibu na kamati ya maandalizi," amesema Bach. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha