

Lugha Nyingine
Mradi mkubwa wa kusambaza maji wa China wanufaisha watu milioni 140
![]() |
Picha iliyopigwa Mei 22, 2021 ikionesha mfereji wa maji wa Shahe, mradi muhimu wa njia ya kati ya Mradi wa Usambazaji wa Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini wa China. (Xinhua/Liu Shipping) |
BEIJING - Mradi mkubwa wa China wa kuchepusha maji umesafirisha karibu mita za ujazo bilioni 50 za maji kutoka mito mikubwa ya Kusini hadi maeneo ya Kaskazini yanayokabiliwa na ukame katika kipindi cha miaka saba iliyopita.
Jumapili ya wiki iliyopita ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka saba tangu ujenzi wa Mradi wa Kusambaza Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini. Mradi huo umewanufaisha watu milioni 140 na kuboresha muundo wa maendeleo ya uchumi wa zaidi ya miji 40 mikubwa na ya kati.
Kwa mujibu wa Afisa kutoka Wizara ya Rasilimali za Maji, mradi huo umebadilisha mfumo wa usambazaji maji Kaskazini mwa China, umehimiza urejeshaji wa uhai wa mito na maziwa ya maeneo na kurekebisha muundo wa viwanda, na kutoa faida kubwa za kiuchumi, kijamii na kiikolojia.
Mradi wa Kusambaza Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini una njia tatu. Njia ya kati, iliyo maarufu zaidi kati ya hizo tatu kutokana na kusambaza maji kwenye Mji Mkuu wa China wa Beijing, inaanzia kwenye Bwawa la Danjiangkou katikati mwa Mkoa wa Hubei nchini China na kupita Henan na Hebei kabla ya kufika Beijing na Tianjin. Ilianza kusambaza maji mnamo Desemba 12, 2014.
Njia ya Mashariki ilianza kufanya kazi mnamo Novemba 2013, kusambaza maji kutoka Jimbo la Jiangsu Mashariki mwa China hadi maeneo ya kupokea maji ikiwa ni pamoja na Tianjin na Shandong.
Njia ya Magharibi iko katika hatua ya usanifu na bado haijajengwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma