Dondoo muhimu za Olimpiki ya Majira ya Baridi: Nini tofauti kati ya kuteleza kwa kasi na kuteleza kwa kasi katika mduara mfupi kwenye barafu?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2021

Tofauti kubwa kati ya mbio za kuteleza kwa kasi na mbio za njia fupi za kuteleza kwa kasi kwenye barafu ni urefu wa mzunguko, urefu wa njia ya kuteleza kwa kasi ni mita 400 kwa mzunguko mmoja wakati kuteleza kwa kasi kwa njia fupi ni mita 111.12.

Njia ya mzunguko wa kuteleza kwa kasi kwenye barafu ina njia ya ndani na ya nje, na ubadilishaji wa njia hutokea mara kadhaa katika mashindano. Njia ya mzunguko ya kuteleza kwa kasi ya njia mfupi haina njia ya ndani au ya nje, lakini ina alama nyeusi za vizuizi za mpira vilivyowekwa pembeni, kama ukumbusho kwa watelezaji kwenye barafu kwamba lazima wasivuke mstari. Hakuna mistari ya alama kando ya njia ya moja kwa moja na watelezaji kwenye barafu wanaweza kusonga mbele kwa uhuru.

Wakati wa mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa kasi, watelezaji huvaa vifaa vya kuteleza kwenye barafu, blade na buti zikiwa zimetenganishwa, wakati watelezaji kwenye wa mbio za njia fupi za kuteleza kwa kasi, huvaa buti za kuteleza kwenye barafu ambazo huwa na blade ambazo ziliwekwa nje ya katikati upande wa kushoto badala ya kuwekwa katikati,na zimekunjika kwenye tao ili buti zisiguse barafu wakati watelezaji wanaegemea eneo la kugeuka.

Pia, watelezaji kwenye barafu kwa kawaida huvaa suti zinazokabiliana na upepo wakati wa mbio za kuteleza kwa kasi, wakati wa mbio za njia fupi za kuteleza kwa kasi, watelezaji huvaa glavu zinazozuia majeraha, miwani ya kinga ya michezo, na kofia ngumu, miongoni mwa vifaa vingine.

Idadi ya wanamichezo kwenye mbio za kuteleza kwenye barafu pia ni tofauti. Katika mbio za mtu mmoja-mmoja za kuteleza kwa kasi, watelezaji wawili hukimbia kwa wakati mmoja, huku katika mbio za njia fupi za kuteleza kwa kasi kwenye barafu, watelezaji sita wa timu mbili hukimbia kwa wakati mmoja. Katika mbio za njia fupi za kuteleza kwa kasi kwenye barafu, idadi ya wanamichezo wanaoteleza ambao hushindana katika mbio za mita 500 na 1000 kwa kawaida ni watelezaji wanne, huku idadi ya watelezaji wanaoteleza katika mbio za mita 1500 au zaidi huanzia sita hadi wanane.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha